Friday 28 October 2016

MKUBWA FELLA AJA NA YAH TMK MODERN TAARAB



NA SALEH JUMA
Kituo cha mkubwa na wanawe kilichopoTemeke jijini DAR ES SALAAM hivi karibuni kimeunda bendi mpya ya miondoko ya taarabu inayofahamika kama YAH TMK MODERN TAARABU iliyopo chini ya mkurugenzi Saidi Fella.
 
Fella amesema aliamua kuunda bendi ya taarabu baada ya kuona wasanii wazuri na wakali kutoka bendi ya jahazi modern taarabu kujiengua katika bendi hio hivyo aliona ili kuendeleza mziki wataarabu na kuendelea kuutangaza nje ya nchi ni vyema kuunda bendi ikiwa ni moja njia ya ajira kwa vijana hao pia kuutangaza mziki huo.

Aidha aliwataja wasanii walio jiengua katika kundi la jahazi na kuunda bendi mpya ya ya yah modern taarabu kuwa ni Fatma Mahmod (mcharuko), Aisha vuvuzela,Chidy boy, Kichupa, Mussa Mipango na Mohamed Mauji pia wasanii wengine waliojiunga na bendi hio kutoka bendi nyengine tofauti ni Maua Tego na Omary Tego ambao awali walikua wanaunda kundi la Coast Modern Taarab.
 
Pia amewaomba watanzania kuipokea kwa mikono miwili bend yake hio mpya na kutoa sapoti ya kutosha kwa kununua kazi zao kuomba katika media tofauti nyimbo zao kucheza na kujitokeza kwa wingi katika maonyesho yao.
 
Lakini pia amewa ahidi kuwapatia burudani za kutosha watanzania kwani bendi tayari ipo kambini na tayari wameshaingia studio kurekodi  nyimbo mbili ambazo mwisho mwa wiki hii zitaanza kusikika katika media tofauti.



SERIKALI YALALAMIKIWA JUU YA UPANDISHWAJI WA KODI



NA SALEH JUMA

Wafanyabiashara wa   soko dogo    lililopo kinondoni manyanya wamelalamika juu ya kukosekana kwa wateja  na biashara  kuwa mbaya kutokana na kupandishiwa kodi na bidhaa kuuza kwa bei yajuu.
Ndugu Saidi Abdallah ambaye ni mfanyabiashara wa vifaa vya simu katika soko hilo alisema kuna upungufu mkubwa wa wateja katika biashara yao ambayo tofauti na mwaka mmoja nyuma.
 
“Mwaka jana na mwaka huu biashara iko tofauti kabisa kwani unaweza kufungua duka tokea asubuhi mpaka saa saba bado hajapita mteja kodi imepanda halafu pia bidhaa huko tunapo nunua kwa jumla bei ipo juu na sisi tunapo uza wateja wanalalamika”

Aidha kwa wafanyabiashara wa vyombo vya plastic nao wamesema kwa upande  wao biashara ni ngumu kwani ushuru wa kuingiza vyombo ni mkubwa kwa hivyo mpaka inafika kuuzwa chombo dukani kwa bei yake inakua ipo juu kidogo hivyo wateja wengi wamekua hawaonekani mara kwa mara kujipatia mahitaji yao.
 
Kwa upande wa wafanyabiashara wa vyakula kama vile ndizi,mihogo,na viazi wamesema kwa upande wao kidogo biashara imekua afadhali nzuri kwani wateja hufika mara kwa mara kununua bidhaa kwaajili ya chakula kwani kula ni muhimu kwa mwandamu hivyo hakuna sababu inayomfanya  mwanadamu kushindwa kula hata kama maisha yapo juu.
 
Lakini pia wameiomba serikali kupunguza kodi kwa wafanyabiashara ili waweze kujimudu kimaisha kwani wengi wa wafanyabiashara ni wanafamilia na zinawategemea na biashara ndio kila kitu kwao wanazo zitegema ili kumudu maisha yao.

WATANZANIA WASHAURIWA KUFUATA UZAZI WA MPANGO




NA SALEH JUMA

Watanzania washauriwa kufuata uzazi wa mpango na uzazi salama ili kupunguza ama kuondoa kabisa tatizo la watoto wa mitaani linalotokana na wazazi kuto kumudu familia zao kwasababu  ya hali ngumu ya umasikini.

Hayo yamesemwa oktoba 25 na naibu waziri wa afya katika warsha ya siku mbili ya wadau mbalimbali wa sekta ya afya iliofanyika katika baraza la maaskofu kurasini jijini DAR ES SALAAM

“Wazazi na watanzania wenzangu tujitahidi kupanga uzazi salama ili kupunguza kabisa tatizo la watoto wa mitaani kutokana na ugumu wa maisha tunashindwa  kumudu familiazetu”

Aidha amewataka watanzania kujitokeza kupima virusi vya ukimwi ili kujua afya zao na kuanza tiba mapema endapo amegundulika kuwa tayari ameambukizwa virusi vinavyo sababisha ukimwi kwasababu serikali inatoa huduma hizo bure bila malipo yeyote.
 

ZEBRA KROS YAPUNGUZA AJALI TSJ



Na Fikiri yusuph abdallah
Chuo cha uandishi wa habari tsj kilichopo ilala bungoni mtaa wa sharifu shamba jijini dare s salaam    kimeamua  kuchukua uamuzi wa kuweka alama za barabarani zebra krosi kwa dhumuni la kupunguza ajari ambazo zimkuwa ziktokea mara kwa mara katika maeneo hayo.
 Image result for ZEBRA CROSS
Baada yakufanyika kwa zoezi hilo kwa sasa baadhi ya ajali zimepungua katika maeno hayo kwa kiasi wakati hapo awali baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho na watembea kwa miguu walikua wakipata ajali kwa kiasi kikubwa sana waliweza kupoteza maishakutokana na baadhi ya  madeleva  wakiwa wanaendesha vyombo vya moto.

Image result for ZEBRA CROSS

UJENZI WA BARABARA YA TAZARA WAVUNJA REKODI



Na Fikiri yusuph abdallah
Ujenzi wa barabara ya nyerere road iliyopo tazara jijijni dar s salaam mpaka sasa imewez kuvunja rekodi kwa kiasi kikubwa sana,ujenzi wa barabara hiyo kila kukicha inaleta mtumaini y watanzania wngi

 
Wakandalasi wa barabara hiyo wamesema wanahitaji kufanya kazi usiku na mchana  ili mladi huo uweze kumalizika  kwa mda ambao waliokubaliana na serikali ya Tanzania.

Pamoja  na wafanyakazi wa barabara hiyo wanajitaidi kufanya kazi kwa bidii kwa dhumuni la kuweza kufanikisha  ujenzi huo kwa haraka zaidi ili watu na watanzania kwa ujumla waweze kunufaika na mladi huo
 
Hivyo basi,japokuwa ujunze huo na changamoto za msongamano wa magari lakini mafundi na makandalasi wanajitaidi kufanya kaazi kwa nguvu.