Na Christian John
Baada ya mgogoro wa muda mrefu bain ya
serikali na wakazi wa Tegeta machimbo ya mawe sakata hilo limehamia kwa Mbunge
wa Jimbo hilo la Kawe Mh.Halima Mdee na kuzungumza na wananchi wa maeneo hayo.
Akizungumza hayo katika ziara aliyoifanya eneo
hilokwa lengo la kujua matatizo yanayowakabili wananchi wake Mdee amewatia moyo
kwa kuwaambia atapigana kwa kadiri anavyoweza kuhakikisha wanapata haki yao.
"Wanasema nyie ni wavamizi lakini hakuna
mvamizi kwenye nchi yake nyie mna haki ya kuwa hapa kuna watu wana miaka zaidi
ya ishirini maeneo haya wameoa na wana wajukuu
nyie niwamiliki halali kabisa"
Baada ya kuulizwa kuhusu kauli hiyo na huenda
ikamletea matatizo kwa kuikashifu serikali alisema
"Hakuna wa kuikashifu serikali wala
kuidharau ila tunaongea ukweli ambao upo wazi kabisa ili mradi hatujatukana
basi tujue wazi tuna haki"
Kwa muda mrefu sasa serikali imekuwa katika
mgogoro na wakazi wa eneo hilo kwa kile kinachodaiwa wakazi hao kuvamia eneo
hilo ambalo halijapimwa na manispaa.
No comments:
Post a Comment