Thursday 27 October 2016

GEST HOUSE ZA SHAMIRI DAR ES SALAAM

Na Yasinta Mkonyi Dar

Wakati serikari ikifungia baadhi ya sehemu za starehe na hoteli mbalimbali jijini Dar es Salaam kwa kutokulipa kodi. Baadhi ya mitaa imeonekana ikiendelea na ujenzi wa nyumba za kulala wageni maarufu kama Gest Bubu.
 Akizungumza kwa masikitiko makubwa mwenyekiti wa mtaa wa Ubena katika kata ya Gongo la Mboto bwana Sultan Said jana kwenye mkutano ulioitishwa kwa wajumbe wa nyumba kumi. Alisema ameamua kuitisha mkutano huo ili kujadili mambo ya mitaa yetu yanayoendelea kutokea likiwemo suala zima la ongezseko la nyumba za kulala wageni maarufu kwa jina la Gest House katika makazi yetu.

 Alisema; ameamua kuitisha mkutano na wajumbe wa nyumba kumi ili kuweza kujadili ni jinsi gani ya kufanya maana wajumbe wa nyumba kumi ndio wanaofahamiana na wamiliki wa nyumba hizo. Aliondelea kusema kuwa inawezekana waliofungiwa hoteli hizo kubwa wengi wao ni wamiliki wa nyumba hizo zinazojengwa za kulala wageni kwa maarufu kwa jina la Gesti House ili kukwepa kulipa kodi.

Aidha, bwana Sultani aliongeza kusema kuwa atahakikisha baada ya kupata idadi kamili ya nyumba hizo kupitia kwa wajumbe hao wa nyumba kumi zilizopo katika mtaa huo, atahakikisha zinajulikana na serikali ili waweze kuwa na leseni na viambatanishio kutoka katika serikali ya mtaa. Kinyume na hapo hazitaruhusiwa kufanya kazi mpaka zitakapokidhi masharti na vigezo husika.
Baadhi ya wajumbe hao wa nyumba kumi waliweza kupata fursa ya kutoa maoni yao huku wakionekana wakimuunga mkono maamuzi ya mwenyekiti huyo wa Ubena.
Pia mwandishi wetu aliweza kupata fursa ya kuongea na baadhi ya wananchi wa mtaa huo juu ya hatua ambazo zimechukuliwa na serikali ya mtaa wa Ubena. Bi. Anna alisema kuwa anafurahishwa sana na hatua hiyo iliyochukuliwa katika kudhibiti nyumba hizo maana zimekuwa kero katika mtaa wao huku akiiomba serikali iweke mkakati kamili katika kudhibiti watoto ili waweze kuzuiliwa kuinguia katika nyumba hizo.



No comments:

Post a Comment