Na Mari
Kilua
Swala la
wazawa kutembelea vivutio bado imekuwa changamoto ndani ya hifadhi nyingi
nchini Tanzania pamoja na kwamba Tanzania ni moja ya nchi zinazoongoza kwa
vivutio vingi vya utalii
Akizungumza
na waandishi wa habari kutoka Tsj mmoja kati ya waongoza wageni ndani ya
hifadhi ya Ngorongoro George Okol amesema "tumekuwa tukipokea watalii wa
kigeni zaidi kuliko wazawa na hii inaonesha ni jinsi gani watanzania
tunashindwa kijani kujari cha kwetu".
Pia mmoja wa
watalii wa ndani ambaye alikuwa ndani ya hifadhi hiyo amesema "kiukweli
inatia aibu sana kwa swala la wageni kuwa wengi kuliko wazawa, cha msingi
serikali pamoja na waandishi mnatakiwa kufikisha elimu ya kutosha kwa
watanzania ilikuweza kutoka kwenye janga hili", amesema mmoja ya watalii
ambaye hakutaka kutaja jina lake.
Baadhi ya
wazawa wameileza jsj kuwa sababu inayowafanya washindwe kutembelea hifadhi zao
ni kutokana na bei kubwa ya kiingilio ikijumulishwa na pesa ya kulipia kula
kitu ndani ya vivutio hivyo
Nayo mamlaka
ya hifadhi ya taifa ya utalii imeeleza kuwa watajiatahidi kupunguza kiingilio
kwa watalii wa ndani ili kuweza kuwatia moyo zaidi watalii hao.
No comments:
Post a Comment