Wednesday 26 October 2016

WANANCHI WALALAMIKIA UWEPO WA MALORI MTAANI

Na Richard Y Kasaini

Wananchi wa mtaa wa Sharifushamba wamelalamikia uwepo wa malori na mabasi yanayoizidi uwezo barabara iliyopo mtaani hapo.Wakizungumza na chombo hichi wengi wameonekana kuchukizwa na uwepo wa malori na kusababisha msongamano usio na maana katika barabara hiyo.
BASI LINALOMILIKIWA NA KAMPUNI YA SARATOGA LIKIWA LIMEEGESHWA NJIANI

Mtaa wa sharifushamba ni moja kati ya mitaa yenye bahati kujengewa barabara zenye kiwango cha lami.Kutokana na uwepo wa malori na mabasi makubwa na kukosekana kwa maegesho ya magari kupita katika barabara hiyo,hivyo imekuwa kero kwa baadhi ya watumiaji wa barabara hiyo hasusani wakazi wa maeneo hayo.
Baadhi ya wananchi wanaokaa katika mtaa huo wameeleza kero yao kubwa huku mmoja kati yao ambaye anafahamika kwa jina la Munga jina kamili Said Munga alisema kuwa kero yake kubwa ni uwepo wa malori yaliyozidi uwezo wa barabara hiyo kwani barabara hiyo imejengwa maalumu kwa magari yenye tani 10 mpaka 15 lakini cha kushangaza mpka mabasi makubwa yanapaki na kupakia mizigo eneo hilo.
LORI LINALOMILIKIWA NA KAMPUNI YA BACK TOWN LIKIJARIBU KUPITA KATIKA BARABARA HIYO AMBAYO IKO MTAANI AMANA SHARIFUSHAMBA PEMBEZONI KUNA MAKAZI YA WATU
Baada ya kuzungumza na wananchi nikapata nafasi ya kuongea na mmja kati ya madereva wa mabasi yanayomilikiwa na kampuni ya SARATOGA ambayo hufanya safari zake za kutoka Dar es salaam kwenda Kigoma alisema kuwa kampuni hiyo ipo hapo kwa muda mrefu na yeye hafahamu lolote juu ya barabara hiyo kwani yeye sio mkaaji sana kwani huwa anasafiri mara kwa mara.

BAADHI YA MAGARI YAKIWA YAMEEGESHWA PEMEBEZONI MWA BARABARA INAYOPITA MTAA WA AMANA SHARIFUSHAMBA

Hata hivyo kutokana na uwepo wa nyumba ya kulala wageni jirani na eneo hilo na ukizingatia nyumba hiyo haina sehemu ya kuegeshea magari na hivyo kupelekea msongamano ambao mara nyingi huwa nio kero kwa watumiaji wa barabara hiyo kwani barabara hiyo ni nyembamba sana.Hivyo ilinibidi kuzungumza na mmiliki wa nyumba hiyo lakini juhudi za kumpata ziligonga mwamba.

No comments:

Post a Comment