NA ANNA J. MUNISI
Wananchi na
wakazi wa jiji la Dar es salaam hasa
wale wanaotumia barabara ya TAZARA wamefurahishwa na kitendo cha serikali kutekeleza ujenzi wa
barabara hiyo ambayo ilikuwa ikilalamikiwa
kuwa na adha kubwa ya foleni.
Awali
wananchi na madereva wanao tumia barabara hiyo walikuwa wakipata shida sana
kupita katika barabara hiyo kutokana na msongamano mkubwa wa magari na hivyo
kuchelewa mahali wanapokwenda.
Akizungumza
na mwandishi wetu mmoja waabiria alisema
“ unajua sasahivi wanatupa moyo kidogo kwa kuuona ujenzi wa barabara mpya
nadhani itatusaidia sana siku za mbeleni kwani tumekuwa tukifika majumbani
usiku sana kutokana na eneo hili kuwa na foleni kubwa” alisema mmoja wa abiria ambaye hakutaka jina lake
lifahamike.
Naye Bw.
Hashim Kareem alisema “tunatamani sana ujenzi huu ukamilike ili foleni
zipungue, watu wanachelew kazini na wengine wanafika nyakati za usiku sana
majumbani hii si nzurio kwani tunahatarisha maisha yetu kutokana na vibaka
ambao wanazurura usiku”.
Aidha mmoja
ya wakandarasi wa eneo hilo Christian Joseph amabae anashughulika na
ujenzi huo wa barabara alitoa ufafanuzi
kuhusiana na barabara hiyo ya TAZARA
kuwa ujenzi utakamilika ifikapo mwaka 2018 na barabara hizo zitakuwa ni
za juu na chini ili kupunguza foleni ya magari, kutakuwa na barabara maalumu
kwaajili ya magari makubwa na nyinginekwaajili ya magari ya kawaida.
No comments:
Post a Comment