Thursday, 27 October 2016

USALAMA WAHIMARISHWA KWA WAENDESHA BODABODA JIJINI DARE S SALAAM

., Tamriha Hamisi
Dar es salaam
                           
Kutokana na hali ya ongezeko la ajali mara kwa mara za waendesha bodaboda  ikionekana kuwa na kasi kubwa ndipo polisi walivalia njuga suala wahimarisha usalama kwao katika maeneo mbalimbali jijini Dar es salaam

Baadhi ya wakazi katoka maeneo mbalimbali walipongeza jeshi la polisi la usalama bararani kwa kazi nzuri ya kuhimarisha usalama kwa waendesha bodaboda wakisema kuwa watapunguza ongezeko la ajali na usalama wao kiujumla.

Safari 255 ilijaribu kulivutia waya polisi wa usalama barabarani na kupata nafasi ya kuongea na mmoja kati yao kwa sharti la kutotaja jina lake kwa usalama zaidi akithibitisha kuwa wanashukuru kuwa mpango wao umefanikiwa kwa kuwa sheria zinafatwa na elimu waliyotoa imezingatiwa.

Mwenyekiti wa waendesha bodaboda katika eneo la Tazara akili kuwa wamepewa elimu ya kutosha ambayo imewashawishi wao kuwa katika hali nzuri ya usalama na kazi yao ya kujitafutia ridhiki za kila siku Alisema Juma Rajabu.

Akizungumza na Safari 255 Abiria kuwa imekuwa changamoto kwao katika safari zao katika shughuli za kila siiku na imewafanya wawe makini kwa kuzingatia kupanda bodaboda ambayo inakidhi vigezo vya sheria maana ukiwa mzembe ulipa faini  ya sh.30000 kwa uzembe.


No comments:

Post a Comment