NA NAJAT ATHUMANI.
WAKAZI wa
eneo la Spenko Vingunguti wamelalamikia uongozi wa eneo hilo kwa kuto kupuliziwa
dawa kwenye mabwawa ya maji taka jambo
linalopelekea kugeuka mazalia ya mbu pamoja nakutoa harufu kali wamesema hayo
walipo tembelewa na mwandishi wetu jana.
Wamesema
kumekuwa na kawaida ya baadhi ya viongozi wanao husika kulipuuzia swala hilo
kwa kutokufuata utaratibu ulio wekwa na serikari wa kuhakikisha mabwawa yanapuliziwa dawa kila baada ya muda mfupi
swala linalopelekea kero kubwa kwa wakazi hao.
"Mwanzoni
walikua na utaratibu mzuri walikua
wanapulizia dawa kila baada ya muda mfupi lakini sasa wamekuwa wanafanya wanapojisikia
swala linalokua kero kwetu hasa nyakazi za mchana jua linapo waka hua kunakuwa
na harufu kalii na nyakati za usiku mbu wanakuwa wengi mno” alsema
mmoja wa wakazi wa eneo hilo anayejulikana kwa jina la Elizabeth Mlawa.
Naye mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo Bw Omary
said Omary naye alikua na haya yakusema "mimi napokea malalamiko mengi
mpaka nakosa raha nikweli kunatatizo hilo namimi najitahidi kadri ya niwezavyo
kulishugulikia napia kumekua na mzunguko mkubwa wa kupatatikana kwa dawa hizo
mwanzo kulikuwepo shiriika kutoka marekani lililo kuwa na kampeni ya kuzui
Malaria ambalo ndio lililokua linapulizia dawa hivyo baada yakuondoka kumekua
nashida kwakweli". alisema
Juhudi bado zinaendelea za kumtafuta meya wa jiji kutolea ufafanuzi wa
kina juu ya suala hili linalowakerehesha wakazi wa spenko kwani mbu wanaozalishwa
na bwawa hilo wanachangia kwa kiasi kikubwa kusabisha kuongezeka kwa idadi ya
maambukizi ya ugonjwa wa malaria hasa kwa watoto chini ya miaka mitano na wamama
wajawazito.
Baadhi ya wakazi wa spenko
wakiendendea na shughuli zao za kila siku pembezoni mwa mabwawa ya maji taka
Picha ikionesha muonekana halisi wa
mabwawa ya maji taka yaliyopo vingunguti mtaa wa spenko.
PICHA NA NAJAT ATHUMANI.
No comments:
Post a Comment