Na ANITHA JAIL
Wafanyabiashara ndogo
ndogo(machinga)wamepatwa na sintofahamu baada ya wagambo wakishirikiana na
polisi kuwafukuza katika maeneo ambayo sio sahihi kufanyia biashara
Machinga washatangaziwa
kuacha kufanya shughuli zao kwa kupanga barabarani hususani barabara ya mabasi
yaendayo haraka katika mitaa ya Kariakoo na Mnazi mmoja ili kupunguza
msongamano wa watu mjini
Wafanyabiashara wamepata
hasara ya vitu vyao kwani Polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi ili
kuwaondoa katika eneo hilo
Wagambo wa jiji
wakishirikiana na mapolisi wametanda kila kona ya mitaa ya Kariakoo kupambana
na machinga ambao wameambiwa wahame maeneo hayo
Baada ya tamko hilo wamachinga wamekataa
wamedai haiwezekani tutapambana nao kwani hawana maeneo ya kufanyia bishara zao
Licha ya vitu vyao kuharibiwa
baadhi ya machinga walipata majeraha katika harakati za kuokoa mali zao
‘Nategemea na napoteza muda mwingi kufanya biashara hii
kukidhi mahitaji ya kifamilia na kusomesha watoto wanavyotufukuza hatuna sehemu
nyingine ya kufanyia biashara’Alisema mmoja wa wafanyabiashara hao
No comments:
Post a Comment