Na Sabore Laizer
Chuo cha
Uandishi wa habari Time school of journalism kilichopo jijini Dar es salaam
kilitembelea shule ya msingi LAIBONI iliyopo kata ya makuyuni wilaya ya Monduli
mkoa wa Arusha na kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa mwanafunzi .
Mratibu wa
masomo katika chuo cha Tsj Bi Blandina Semaganga alisema serikali ya mwanafunzi
ikishirikiana na uongozi wa Chuo iliandaa zawadi kidogo kwa ajili ya mwanafunzi
ikiwemo madafutari kalamu box sita, katoni nne, sabuni katoni tano, na sabuni
ya unga box moja lenye zaidi ya vipande miamoja .
Mkuu wa
shule hiyo Bi Rogath mbuya alishukuru uongozi wa chuo cha Tsj kwa msaada
hiyo,vilevile alibanisha changamoto mbalimbali katika shule ya ke kuwa
wanatatizo la maji has a kipindi hiki cha kiangazi wanalazimika kununua maji
kwa ajili ya matumizi ya shule.
Bi mbuya
aliongeza kuwa boza ya Lita mia tatu inagharimu shilingi laki mbili kutoka Mto
wa mbu ambapo maji hayo yanatumika katika shughuli mbalimbali shuleni hapo
ikiwemo kupikia ,kudeki madarasa na usafi vyooni.
Pia Bi mbuya
alisema kuwa wanapata pesa ya kununua maji kupitia michango kwa wazazi na
wafadhili kutoka sehemu mbalimbali na vile vile pindi maji yanapokosekana
shuleni mwanafunzi hushinda njaa kuanzia saa moja asubuhi hadi saa kumi jioni
watakaporudi nyumbani.
Licha ya
kukumbana na changamoto mbalimbali shule ya LAIBONI ni ya kipekee ambapo
ilianzishwa 1997 na Mganga wa jadi Mzee Meshuko Mapi kwa ajili ya familia take
na watoto wa jirani.
No comments:
Post a Comment