Thursday, 27 October 2016

VIONGOZI WA CHADEMA WATEMBELEA WANANCHI JIMBO LA KAWE



Na Christian John
Baada ya kuchaguliwa na madiwani kuwa Meya mpya wa manisapaa ya Kinondoni hivi karibuni Mstahiki meya wa manispaa ya kinondoni  Boniface Jacob ameanza kuonyesha umma kuwa anajali wananchi kwa kufanya ziara na mbunge wa Kawe Mh.Halima Mdeejimbonihumo.
Akizungumza na wananchiMh.Halima Mdee amewaambia wananchi kuwa lengo kubwa la ziara hiyo ni kuona ni na kujadili matatizo wanayokumbana nayo wananchi kila siku na serikali yake kuona ni namna gani inaweza kuyakabili.
“Hatufanyi ziara za kutumbua majipu ila tunataka kuona matatizo ya wananchi na kujadiliana maendeleo ndiyo lengo kubwa”
Naye Mstahiki  Meya wa manispaa ya Kinondoni  Jacob Boniface amewashukuru wakazi wa kawe kwa kumuamini Halima Mdee na kumchagua tena kuongoza jimbo hilo huku akiwatoa wasiwasi kwa maneno yanayozagaa kuwa hawezi kuongoza Manispaa ya Kinondoni kwa kigezo yeye si mzoefu.
“Hata Magufuli pia si mzoefu wa Urais ila amepita na tunaheshimu maamuzi yake sasa hata mimi pia najua ntaongoza kwa uaminifu na weledi mkubwa hayo maneno mengine hayana maana yoyote tushirikiane kufanya maendeleo”
Mstahiki Meya wa Kinondoni aliendelea na ziara hiyo hadi Bunju na kufikia kwenye ofisi za serikali ya mtaa Bunju B.


No comments:

Post a Comment