Thursday 27 October 2016

Baadhi wapongeza uongozi wa serikali yabwanafunzi (TISJOSO)

Na Maria Kilua

Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari (Tsj) wametoa pongezi kwa uongozi wa serikali ya wanafunzi  (TISJOSO) kwa kuweza kukabiliana na changamoto zilizowakabili baadhi ya wanafunzi walioudhulia safari ya kimasomo (study tour)ilyofanyika jijini Arusha.



Akizungumza na mwandishi wetu mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho aliyejitambulisha kwa majina MARY PETER amesema kuwa licha ya changamoto kuwa nyingi wakati wakati wa safari hiyo walifika salama na kufanikisha kurudi nyumbani salama kutokana na uongozi mzuri uliopo a wangu hii, kweli mwaka huu ni kazi tu.


Pia Prosper Kaijage ambaye ni waziri wa elimu mstahafu amesema "kiukweli changamoto zilikuwa nyingi sana kwanza tumingia sehemu chakula bei juu, tukakafika Manyara na kulala kwenye magari kutokana na kukuta vyumba vimejaa lakini viongozi walijitahidi kwa kweli mpaka kufanya watu tusahau shida.., yaani safari hii tumeinjoyi.



Nae katibu mkuu wa serikali ya wanafunzi Shinuna Swale ameongezea kwa hayo "ushirikiano, busara na maamuzi ya kwa pamoja ndio sababu kubwa ya matokeo hayo ila, kiukweli  tuna haki ya kupongezwa.

No comments:

Post a Comment