NA NAJAT ATHUMANI.
Wafanya
biashara wa eneo la buguruni wameishukuru serikali kwa kufanikisha ujenzi wa
kivuko cha juu kilichomalizika mwishoni mwa wiki jana jambo linalowasaidia
wakazi hao kuvuka kwa urahisi kutoka upandemmoja kuelekea mwingine bila bugudha
yoyote.
Mwandishi
wetu alishuhudia hayo alipotinga eneo
ambalo lipo daraja hilo ili kushuhudia
na kupata maoni ya wananchi kuhusu kivuko hicho huku wengi wakionesha furaha
yao kwa utekelezaji wa jambo hilo.
‘‘ Kivuko hiki kimetusaidia sana kwasababu
tulikuwa tunapata shida kuvuka barabara kutokana na kasi ya madereva wa vyombo
vya moto mara nyingi wanapita kwa kasi sana kwakweli serikali imetuona’’alisema
mmoja wa wafanyabiashara waeneo hilo anayejulikana kwa jina la Sayde Othuman.
‘‘ hiki
kivuko ni chetu tumejenga kwa kwa kodi zetu lakini cha kushangaza wachache
watakitumia vibaya ndani ya mwezi tu
wataanza kung’oa vyuma serikali iangalie
hilo sio kwasababu wamemaliza basi wakiiche tu watu tunatofautiana uelewa’’
alisema Michael Kasoni mkazi wa
buguruni.
Pia
tuliongea na askari wa barabarani aliyekuwa zamu kuongoza magari eneo hilo alisema eneo hilo
huwa linakluwa na foleni kubwa jambo linalowafanya wavukaji kuvuka pindi magari
yanapokuwa kwenye foleni huku waendesha pikipiki wakipita kwa kasi pembezoni
mwamagari hivyo kuhatarisha maisha ya wananchi wanaovuka katika hiyo barabara.
‘‘boda doda
wanakatisha kwa kasi pembezoni mwa magari yakiwa yamesimama kusubiri ruhusa mtu
akikatisha vibaya lazima apitiwe na pikipiki,kwasasa kuna nafuu maana wanafunzi ndio walikuwa
wanapata shida kuvuka sasa wanapanda tu kivuko wanavuka kirahisi wahusika
wamejitahidi na mimi wito wangu ni kwa wananchi kukitunza kivuko hicho na siyo
hicho tu bali na miundombinu yote inayotusaidia hasa ya barabarani ili iweze
kutusaidia’’ alisema askari huyo.
Ni siku
chache zimepita tangu kutokea ajali iliyosababishwa na dereva wa pikipiki kugongana na gari kubwa aina ya fuso tukio
lililopelekea bibi aliyekuwa akivuka katika barabara hiyo kugongwa na kupeteza
maisha.hivyo kuwepo kwa ujenzi wa kivuko cha daraja hilo kutasababisha kupungua
kwa ajali.
Hili ni daraja ambalo linatumika kama
kivuko salama kwa wakazi wa buguruni jijini dare s salaam
No comments:
Post a Comment