Na Fatuma Sultani
Chuo cha uandishi wa habari TIME
SCHOOL OF JOURNALISM kilichopo jijini dare s salaam kimepata fursa ya kuajiriwa
sunrise redio pindi wakimaliza masomo yao na pia baadhi ya wanafunzi wamepewa
nafasi ya kuweza kufanya uwandani ndani ya radio hiyo.
Tukio hilo
lilijiri hivi karibuni wakati wanafunzi wa chuo hicho walipokuwa kwenye ziara yao ya kimasomo mkoani
ARUSHA, na kuamua kutembelea kituo hicho cha habari kwa lengo la kujifunza kwa
vitendo zaidi na kuona nini ambacho wenzao huwa wanafanya pindi wawapo
makazini.
Baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho
walifurahi sana kuwepo kwenye radio hiyo kwani
wameweza kujifunza mambo mbalimbali redio hapo,na pia walipata nafasi ya
kuuliza maswali mbalimbali kuhusu fani yao
na walibahatika kuona vitu kwa vitendo.
Mkurugenzi wa radio hiyo alisema
kuwa anashukuru uongozi wa chuo cha TSJ
kwa kuchagua redio yao kwani wamefarijika sana na kuona kuwa kazi
wanayoifanya ni kubwa na jamii huwa wanaikubali na wanaelimika juu ya mambo
wanayoyafanya.
Mkuu wa chuo hicho Bi SUZAN LUKA
alituma salamu za kuwashukuru uongozi wa sunrise redio kwa kukubali ombi lao la
kutembelea kituo hicho na pia kuwashukuru kwa kuonesha ushirikiano wa hali ya
juu ya kuwakubalia wanafunzi kwenda kufanya uwandani redioni hapo kuwaahidi
kupata nafasi pindi wamalizapo elimu ya diploma chuoni hapo.
No comments:
Post a Comment