Wakazi
wa vingunguti jijini Dar es salaam
wamelalamika kwa kukosa kituo cha daladala kwa muda mrefu sasa hali inayopelekea kuwa na wakati mgumu
kipindi wanapokua wanafuata huduma za usafili hususani kipindi cha masika kwa
sababu hulazimika kulowana na mvua kwa kukosa sehemu za kujistili ili wasiweze
kuloweshwa na mvua vilevile majira ya kiangazi hususani mida ya mchana kwa
kuchomwa na jua kali.
Licha
ya kupeleka malalamiko hayo katika sehemu husika na kufanya jitihada kadha wa
kadha ikiwemo kumtumia ujumbe diwani wa
kata hiyo na viongozi wengine lakini jitihada hizo azikuzaa matunda.
Isihaka
Issa mkazi wa vingunguti alikuwa na haya ya
kuelezea dhidi ya kero hiyo
wanayoikumbana nayo ‘’ muda mrefu sasa
tangu sisi wakazi wa huku vingunguti
tuanze kuitumia barabara hii
ambayo ilijengwa bila kuwepo na vituo vya kupumzikia abiria,
Vile
vile Bw. Isihaka Issa aliongeza kwa kusema kwamba tatizo hilo ni sugu kwa
wakazi wa vingunguti na maeneo ya karibu na vingunguti na wote wanao tumia njia hiyo kwa usafiri.
Mwisho
bwana Isihaka alimalizia kwa kuiomba
serikali na mamlaka husika kulitafutia
ufumbuzi swala ili hilo kuwaepusha au kuwaondolea kero hiyo inayo wakabili
katika nyanja muhimu ya usafiri ikiwa ni
pamoja na kuziba baadhi ya mashimo yaliyopo katka barabara hyo inayofahamika
kama kwa buguruni mnyamani.
Mpaka
habari hii inachapishwa jitihada za mwandishi wetu za kukutana na kufanya
mahojiano na uongozi wa eneo hilo
azikuzaa matunda kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu.
Na
msafiri mohamedi
No comments:
Post a Comment