Na Sabore
Laizer
Kituo cha
radio cha Sunrise kilichopi mkoani Arusha kimeahidi kutoa ajira kwa mwanafunzi
wa chuo cha Time School of journalism pindi wakimaliza masomo kwa ngazi ya astashada na stahada .
Akiongea na mwanafunzi
mkuu wa idara ya rasilimali watu mapema wiki hii wakati wa ziara ya kimasoma
bwana Wolter kileo alisema radio inampago wa kuongeza nguvu kazi ili waweze kukidhi
matakwa ya taasisi .
Vile vile
bwana kileo alitoa nafasi kwa mwanafunzi
wa uwandani kwa ngazi ya astashada na stashada na kuahidi kuwa watapata
ushirikiano pindi watakapo kuwa katika mazoezi kwa vitendo "alitoa rai kwa
mwanafunzi wajitume katika masomo kwani wakijitahidi itakuwa rahisi kwao wakati
wa mazoezi" alisema bwana kileo.
Naye Mratibu
wa masomo katika chuo cha Time school of Journalism Bi Blandina Semaganga
alishukuru uongozi wa sunrise radio kwa utayari na ushirikiano walionesha kwa chuo
wakati wa ziara ya kimasomo mkoani Arusha.
Pia Bi Semaganga
aliwahakikishia uongozi wa sunrise kuwa chuo kinafundisha vizuri hivyo
wategemee kupata wanahabari wenye kiu kuhabarisha umma Bi Semaganga aliongeza
kuwa chuo kinafundisha uadishi wa habari kwa nyanja sote yaani
radio,televisheni,magazeti na uandishi
wa mtandaoni.
Baadhi ya mwanafunzi
walishukuru wa serikali ya mwanafunzi na uongozi wa chuo kwa kufanikisha ziara
ya kimasomo katika mkoa wa Arusha kwani imewasaidia wao kujua fursa mbalimbali
,waliofanikiwa kuomba nafasi za uwandani ni Odriani Masawe na Ireni mboya.
No comments:
Post a Comment