NA SALEH JUMA
Wafanyabiashara wa soko
dogo lililopo kinondoni manyanya wamelalamika
juu ya kukosekana kwa wateja na biashara kuwa mbaya kutokana na kupandishiwa kodi na bidhaa
kuuza kwa bei yajuu.
Ndugu Saidi Abdallah ambaye ni mfanyabiashara wa vifaa vya simu
katika soko hilo alisema kuna upungufu mkubwa wa wateja katika biashara yao
ambayo tofauti na mwaka mmoja nyuma.
“Mwaka jana na mwaka huu biashara iko tofauti kabisa kwani unaweza
kufungua duka tokea asubuhi mpaka saa saba bado hajapita mteja kodi imepanda halafu
pia bidhaa huko tunapo nunua kwa jumla bei ipo juu na sisi tunapo uza wateja wanalalamika”
Aidha kwa wafanyabiashara wa vyombo vya plastic nao wamesema
kwa upande wao biashara ni ngumu kwani
ushuru wa kuingiza vyombo ni mkubwa kwa hivyo mpaka inafika kuuzwa chombo dukani
kwa bei yake inakua ipo juu kidogo hivyo wateja wengi wamekua hawaonekani mara kwa
mara kujipatia mahitaji yao.
Kwa upande wa wafanyabiashara wa vyakula kama vile ndizi,mihogo,na
viazi wamesema kwa upande wao kidogo biashara imekua afadhali nzuri kwani wateja
hufika mara kwa mara kununua bidhaa kwaajili ya chakula kwani kula ni muhimu kwa
mwandamu hivyo hakuna sababu inayomfanya
mwanadamu kushindwa kula hata kama maisha yapo juu.
Lakini pia wameiomba serikali kupunguza kodi kwa wafanyabiashara
ili waweze kujimudu kimaisha kwani wengi wa wafanyabiashara ni wanafamilia na zinawategemea
na biashara ndio kila kitu kwao wanazo zitegema ili kumudu maisha yao.
No comments:
Post a Comment