Friday, 28 October 2016

WAKAZI WA ILALA MTAA WA MAFURIKO WALALAMIKIA HARUFU MBAYA YA MTARO

NA ANNA J MUNISI

Wananchi wanaoishi katika eneo la Ilala Bungoni mtaa wa mafuriko wamekuwa wakipata shida kutokana na harufu kali inayotokana  na mtaro mkuu unaopitisha maji taka, na kuitaka serikali kushughulikia suala hilo.

Hali hiyo imekuwa ikiwakera sana wakazi wa maeneo hayo kwani wamekuwa wakivuta hewa chafu napengine kuwasababishia madhara pamoja na magonjwa ya milipuko kama kipindupindu.
Mwandishi wetu alifanikiwa kufika katika eneo hilo na kushuhudia mtaro huo unaotiririsha maji taka na kupata maoni kwa baadhi ya Wakazi wa karibu na mtaro huo.

Bw.Ramadhani Said Mkazi wa eneo hilo alisema “Serikali iangalie kwa jicho la pili japo wametusaidia kuweka Mtaro lakini wameuacha tu inatakiwawaajiri watu kwaajili ya kuusafisha.Unatoa harufu mbaya sana tunashindwa kuvumilia hasa nyakati za mchana” 

“huu Mtaro unatupa shida sana kwanzaunatoa harufu mbaya na pili unazalisha mbu wengi usiku hakukaliki mbu ni wa kutosha.”alisema bw.Ramadhan Said.

Mitaro inasaidia sana kwani inatusaidia kupitisha maji na kupeleka mahala husika pia inasaidia hasa kipindi cha mvua .Hivyo inapashwa kuangaliwa vizur lakini isipotunzwa husababisha magonjwa ya milipuko kama kipindupindu na mazalia ya mbu wzenezao malaria.






No comments:

Post a Comment