Husna Kyelula
Baada ya
kuwasambalatisha Kagera Sugar katika uwanja wa Kaitaba kwa mabao 6-2, na
kuwamalizia kipigi hiko maafande wa JKT Ruvu kwa mabao 4-0, na kutimiza jumla
ya mabao 10, katika mechi mbili.
Yanga baada
ya kuwa na rekodi hiyo kubwa ya magoli imewatisha wapinzani wao Mbao ambao
wanakwenda kukutana nao siku ya jumapili katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es
Salaam.
Katibu wa
Mboa Athanas Machael alisema kuwa hawaogopi rekodi hiyo ambayo Yanga wameiweka
na wanakwenda kushindana na kutaka pointi tatu muhimu kwa mabingwa hao
watetezi.
“Yanga ni timu
kubwa kuliko timu yetu na tunatambua kuwa ndio mabingwa watetezi lakini
hatuogopi kuwa waliweza kushinda jumla ya magoli 10, katika mechi zao mbili
zilizopita”alisema
Pia napenda
kuwaambia wapenzi na mashabiki wa Mbao wakae mkao wa kula na waamini kuwa
tunakwenda kuchukua pointi tatu muhimu dhidi ya mabingwa hao watetezi wa ligi
kuu bara.
Safi sana Dada Husna unajua na umeandika vitu vizuri.
ReplyDelete