Friday, 28 October 2016

MADIMBWI KERO KWA WAFANYABIASHA NA ABIRIA BUNGURUNI SOKONI

NA ANNA J MUNISI.

Wafanyabiashara  wa soko la buguruni na abiria wanaotumia kituo hicho cha daladala walalamikia harufu kali inayosababishwa na madimbwi ya maji yaliyotuama pembezoni mwa kituo hicho. Madimbwi hayo yamekuwa  yakisababishwa na baadhi ya wafanya biashara kumwaga maji machafu katika eneo hilo bila kujali afya  ya watumiaji wa hilo eneo.

 Pia madimbwi hayo yamekuwa kero kubwa  kwa abiria hasa wanaosubiri daladala katika eneo la Bunguruni sokoni  pamoja na wateja wanaoenda kununua baadhi ya matumizi yao kwa kupata shida sehemu ya kusimama na kuchafuka na maji .

Aidha hali  hiyo imekuwa kero kubwa pia hasa kwa madereva wa magari wanaotumia eneo ilo la Bunguruni Sokoni  kwa kupaki gari zao kwaajili ya abiria kwa kulalamikia uharibifu wa magari yao kutokana na mashimo ya madimbwi hayo.

 Akiongea na mwandishi wetu Bw ,Ally Juma dereva wa daladala alisema madimbwi hayo yamekuwa kero kubwa sana katika biashara zao kutokana  na magari  yao kuzima wanapokuwa wanasubiri abiria wanapofika katika eneo hilo.

“haya mdimbwi  bwana yanatupa hasara sana kwanza yanatuharibia magari yetu unakuta unataka kupack  gari inagonga kwenye shimo halafu vifaa vyenyewe  madukani ni gharama sana kwahiyo  tunaishia kununua spea chakavu ambazo zimekwishatumika” alisema


Pia wafanyabiashara wa soko hilo la Bunguruni wamesema sababu ya madimbwi hayo ni kukosekana kwa vitendea kazi vya kufanyia usafi katika soko la Bunguruni na wameiomba serikali kuleta wafanyakazi wakufanya usafi kwenye soko hilo. hali hiyo imekuwa ikiwapa wasiwasi mkubwa  wafanyabiashara pamoja na abiria wa soko la Bunguruni  juu ya madimbwi hayo kwani yanaweza kuwa chanzo kikubwa cha kusababisha magonjwa ya milipuko kama kipindupindu.






No comments:

Post a Comment