Thursday 27 October 2016

"ALIEKOSA NGORONGORO KAPITWA MENGI"

By Shinuna Nassir
Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari Time school of Journalism (TSJ) kilichopo jijini Dar es salaam tarehe 18 ya mwezi wa 10 waliweza kufanya ziara ya kimasomo Mkoa wa ARUSHA ikiwa ni pamoja na kutumia fursa ile kujenga uhusiano mzuri baina ya wanafunzi na viongozi wako.
Ziara hiyo ilifanywa na wanafunzi wasio pungua 70 wakiongozwa na walimu M.wa masomo bi Blandina Semaganga, m.wa wanafunzi bw.George Baltaza  wakishirikana na serikali ya wanafunzi wakiwemo Rais Sabore Laizer makamu wa rais Fatma Sultan sambamba na baraza la mawaziri likiongozwa na Waziri mkuu bw Thomas Ng'itu.
Akizungumza na mwandishi wetu Bi.Maria Kilua ambae ni mwanafunzi wa diploma ya pili akiwa ni mmoja wa waliopata nafasi ya kuwepo katika ziara hiyo alisema amejifunza vitu vingi ikiwemo kuchanganyika na wanafunzi wengine wa ngazi tofauti tofauti lakini kubwa zaidi ni kutembelea hifadhi ya Ngorongoro akisisitiza kwa kusema "aliekosa Ngorongoro kapitwa mengi".
akiendelea kuongea alisema amepata fursa ya kuona wanyama mubashara, kujua tabia zao na sifa zao kwa ujumla, vile vile kujua vivutio vingine kama jamii ya kimaasai ianayoishi ndani ya hifadhi.
Hata hivyo wakiwa ndani ya hifadhi ya Ngorongoro (Ngorongoro creator) waliweza kupata historia ya matukio mbali mbali wakiongozwa na George Okothi na Johaness Japhet (tour guides) ikiwemo Lake Magadi, na wanyama aina tano(the big five animals) waliopo kwa wingi Ngorongorp creater kama simba, Tembo, chui, Nyati na Faru hasa faru weusi.
Akizungumza na gazeti la chipukizi Rais wa serikali ya wanafunzi Bw.Sabore lazier alisema " ni faraja kubwa kwa uomgozi na wanafunzi kwa ujumla kwa mapokezi mazuri walitupokea wenyeji wetu hasa tour guides kutimiza kiu ya baadhi ya wanafunzi walioweza kufika eneo lile kwa niaba yao tunatoa shukran zetu za dhati kabisa"
Aidha mmoja ya waongoza watalii (Tour guide)bw.George Okothi ametoa pongezi kwa wanfunzi na chuo kwa ujumla kwa kuweza kujali na kuthamini vivutio vya nchi na kuweza kuchangia katika sekta ya utalii wa ndani.

No comments:

Post a Comment