NA SALOME MWASAMALE,Dar
SERIKALI imetakiwa kuunda sera maalum
kwaajili ya watu wenye ulemavu wa akili (vichaa, wendawazimu) ili kukabiliana
na unyanyapaa na unyanyasaji dhidi ya kundi hili lililosahaulika.
Hayo yamebainishwa jijini Dar es
salaam na mkurugenzimtendaji wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Focus in
Solution Group (FSG) Mohamed Mchingama alipokuwa akizungumza na jambo leo
kuhusiana na kukithiri kwa vitendo vya unyanyapa na unyanyasaji miongoni mwa
jamii dhidi ya kundi hili maalum.
Mchingama alisema kundi hili
limeshaulika kabisa katika jamii lakini chakushangaza hata serikali imelitenga
kundi hili ambalo pia linahitaji msaada wa hali ya juu.
"Watanzania tunajipanga
kukabiliana na magonjwa mbalimbali kama vile kisukari, kansa, Tb, upungufu wa
damu lakini wakati mwingine tunajiandaa hata kukabiliana na vifo tunasahau
kabisa kukabiliana na ulemavu wa akili (ukichaa na uwendawazimu) na kusahau
kuwa huu ni ugonjwa kama magonjwa mengine na yanaweza kumkuta mtu yeyote katika
maisha", alisema Mchingama
Kwa upande wake mtafiti wa haki za
binadamu katika kituo cha sheria na haki za binadamu (LRHC) Fundikila Wazambi
alikiri kusahaulika kwa kundi hili na kuongeza kuwa hata yeye na taasisi yake
hawajawahi kufanya utafiti kuhusu kundi hili.
“Ni kweli kuwa kundi hili
limesahulika serikali inapaswa kuandaa sera mahususi kwaajili ya kundi hili ili
liweze kutizamwa kwa jicho la tatu na kuangalia namna ya kulinusuru kwa kuwa
unyanyapaa na unyanyasaji dhidi yao umekuwa ukiendelea siku hadi siku”,
alisisitiza Wazambi.
Diwani kata ya Kunduchi Michael Urio akipokea cheti cha
heshima kwaajili ya kuwahudumia watu wenye ulemavu wa akili.Picha na Salome
Mwasamale,Dar
No comments:
Post a Comment