Na Alfredy
Geoffrey Mhagama.
Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari Time school of journalism (Tsj)
kilichopo jijini Dar es salaam wamekuwa na maoni tofauti tofauti kuhusiana na
bei ya vyakula katika ziara yao ya kuelekea
Arusha kufatia beiya vyakula kuwa juu.
[Baadhi wa wanafunzi wa chuo cha Times school of journalism wakiwa wanaelekea hotelini kununua chakula] |
Wakizungumza na mwandishi wetu kwa nyakati tofauti tofautiwanafunzi hao
wameeleza kuwa walipelekwa kula sehemu ambayo bei ya chakula ipo juu ambapo
sahani ya chakula in elfu 3,000hadi elfu 7,000 na kupelekea wanafunzi kutumia
pesa nyingi kwa ajili ya chakula wakiwa njiani korongwe Mkoani Tanga
kuelekea Mkoani Arusha.
Abeli Charles mwanafunzi wa Diploma ya nne katika chuo cha Tsj alisema kuwa
wameshangazwa na kitendo cha viongozi na walimu kuwapeleka katika hoteli za gharama ambapo chipsi kavu ni 3,000 hadi
7,000 hali iliyopelekea kuaribu bajeti yake na mwanafunzi wengine kutokana na fedha
walizopewa in kwa ajili ya Siku zote katika ziara yao ya masomo Mkoani Arusha.
Pia Maria kilua mwanafunzi wa Tsj
Diploma ya pili naye alisema kuwa being ya chakula ilikuwa juu licha ya baadhi ya wanafunzi kwa upande wao
ilikuwa kawaida kutokana na bajeti yao japo kuwa wengi wao waliona being
ilikuwa kubwa tofauti na walivyokuwa wakitegemea licha ya viongozi kuahidi
kuwapeleka sehemu ambayo chakula kitakuwa bei ya kawaida ila haikuwa hivyo.
[Baadhi ya wanafunzi wa Tsj wakinunua chakula katika hoteli ya kilimanjaro wilayani Korongwe Mkoani Tanga] |
Licha ya wanafunzi kulalamikia bei ya chakula baadhi ya wanafunzi kwa
upande wao ilikuwatofauti,Erick Kavishe mwanafunzi wa Tsj BBC first alisema kuwa kwa watu wanaotoka
Mikoa ya kaskazini kununua chakula 3,000 hadi 7,000 katika hoteli mbalimbali ni kawaida ila kwa watu wa Mikoa
mingine kama Dar Es Salaam kwao na kitu cha tofauti.
[Wanafunzi wakipata chakula katika hoteliya kilimanjaro iliyopo Mkoani Tanga] |
Kwa upande wake walimu wa chuo hicho cha Tsj Bwana George alisema kuwa
walilazimika kwenda kula katika hoteli
hiyo kutokana na kuvurugika kwa ratiba na pia wanafunzi kwa muda huo
walitakiwa kupata chakula na kuahidi kuwa watajitaidi kutafuta sehemu ambayo
itakuwa na bei za kawaida za chakula.
Pia Rais wa chuo cha Time School of journalism (Tsj) Sabore Laizer naye alisema kuwa walilazimika kuwapeleka
katika hoteli hiyo kula kutokana na mwingiliano wa ratiba na vilevile
hoteli hiyo ni sehemu ambayo mabasi
mengi yanapitia hapo na abiria kupata chakula hivyo hawakutegemea kukuta bei za vyakula kama zitakuwa juu na kuahidi kutatua
changamoto hiyo.
No comments:
Post a Comment