Na
Fatuma Sultani
Chuo cha uandishi wa habari tsj kilichopo
jijini dare s salaam kimetoa msaada katika shule ya msingi laiboni walipokuwa
kwenye ziara yao
ya kimasomo mkoani ARUSHA.Hiyo ilitokana na wanafunzi hao kuguswa na hali
halisi iliyopo shuleni hapo.
Shule
hiyo ambayo kihistoria ilianzishwa na mzee wa kimasai LAIBONI mwaka 1997
wilayani Monduli kutokana na tatizo lililompata la kufiwa na mtoto wake kwa
ajali ya gari,hivyo kumpelekea mzee huyo kuamua kuanzisha shule yake mwenyewe
ya LAIBONI.
Wanafunzi
wa chuo hicho walitoa msaada wa madaftari,peni,penseli,sabuni na vingine vingi
kwa wanafunzi wasomao shuleni hapo kwani walikuwa wanawasaidia wanafunzi hao
kuweza kuepuka changamoto ndogondogo zitakazowakumba shuleni hapo.
Akiongea
na chombo chetu cha habari mratibu wa masomo wa tsj Bi BLANDINA SEMAGANGA
alisema kuwa wanajisikia faraja sana
kutoa msaada shuleni hapo pia anawapongeza wanafunzi kwa kuwa na moyo wa utoaji kuwasaidia wanafunzi wenzao pindi
wapatapo matatizo,na pia wanajenga uhusiano mzuri na watu wanaowazunguka kwenye
jamii.
.Walimu
mkuu wa shule hiyo Bi.ROGAT MBUYA alisema anashukuru kupata msaada huo kwani ni
kitu cha kiungwana sana,na anaiomba serikali pamoja na jamii ijaribu kuangalia
shule hiyo kwa jicho la tatu kwani wanaupungufu wa madarasa na walimu wanaomba
waongeze na mengine mengi
.
Baadhi
ya wanafunzi wa shule hiyo waliimba na wimbo wa taifa TANZANIA na kumalizia na wimbo wao wa shule wa LAIBONI
LAIBONI
No comments:
Post a Comment