Na
Shinuna
Laiboni ni shule ya msingi inayopatikana
wilaya ya Monduli mkoani Arusha.Shule hii ina historia ya kipekee nchini
Tanzania tofauti na shule nyingine.ni moja ya vivutio mkoani hapo.
Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari
TSJ waliweza kupata nafasi ya kutembelea shule hiyo ikiwa ni moja ya maeneo ya
ziara zao za kimasomo mwezi wa 10.
Akiongea na mwandishi wetu Makamu wa rais
bi Fatma Sultan alieleza kuwa "nia na madhumuni ya kutembelea shule hii ni
kujua vitu vingi kutokana na chanzo cha kuwepo kwa shule hii kusisimua watu
wengi"
Aidha mwalimu mkuu wa shule hiyo
kushirikiana na walimu wengne weliweza kuwapokea wanafunzi hao vizuri na kuweza
kutoa historia ya shule hiyo kwa ufupi.Mwl.mkuu wa shule hiyo bi Rogati Mbuya
alielezea kuwa shule ya msingi Laiboni ilianzishwa na juhudi za mtu mmoja ambae
ni mganga wa jadi kimaasai anaitwa"laiboni"ila majina yake halisi ni
Meshuko Mapii ambae aliweza jenga shule hii mnamo mwaka 1997 kwa madhumuni ya
kuepusha ajali baada ya mtoto wake kugongwa na gari akielekea shule ya msingi
Eslaley ilyoko ng'ambo ya barabara.
Vile vile pamoja na kutolewa elimu katika
shule hiyo kuna changamoto nyingi wanazo kutana nazo walimu pamoja na wanafunzi
hao ikiwemo chakula, maji na kubwa zaidi ni uchache wa madarasa kwani mpka hivi
sasa wanafunzi wa awali wanasoma nje.
Hata hivyo alieleza kuwa pamoja na
changamoto hizo hawajashindwa kuendelea kutoa mafunzo na kujitahidi
kuwafundisha kadri iwezavyo huku akiendelea kujibi maswali ya wanafunzi wa chuo
cha uandishi wa habari time school of journalism, wanachuo wengne walipata
fursa ya kucheza na kuchanganyika na wanafunzi wa Laiboni.
Wanachuo hao wa chuo cha uandishi wa habari
TSJ wakiongozana na mkurugenzi wao wa masomo Bi Blandina Semaganga pamoja na
Mlezi wao George Baltaza hawakwenda mikono mitupu waliweza kutoa baadhi ya
mahitaji kama sabuni, madaftari na kalamu.
No comments:
Post a Comment