Na Peter Mhina.
Abiria katika kituo cha dala dala cha tegeta nyuki wameilalamikia halimashauri ya wilaya ya kinondoni ,kwa kushindwa kukarabati
kituo hicho ikiwa ni pamoja na ukosefu
wa sehemu za kusubiria usafiri ,jambo ambalo limekuwa kero hasa pale mvua inapo nyesha na wakati wa
kiangazi
Akizungumza
kwa nyakati tofauti hapo jana kituoni hapo abiria huyo aliyaelekeza makucha yao kwa viongozi wa halimashauri huku baadhi yao wakiutupia mpira uongiozi wa
kituo hicho kutokana kwa kushindwa kuweka mikakati inayoeleweka kituoni hapo
‘’Nitatizo
kubwa kwasababu ukija kuangalia hakuna sehemu ya kukaa ambayo unaweza kujikinga
na jua ama mvua endepoitakapo kuja kunyesha na muda mwingine unaweza ukaja kuomba wenye vibanda
pembembeni wanaofanya biashara
kujiegama ukawa unawakera vile vile,’’ Alisema mmoja wa abiria hao ,
Pia kwa upande
wa madereva katika kituo hicho wametaka halimashauri kukifanyia malekebisho
upya kituo hicho ikiwa ni pamoja na ubovu wasehemu wanapo paki daladala
kutokana na kuwepo kwa mashimo jambo linalowapa shida wakati wa masika na hivyo kupelekea magari yao kuharibika kila wakati .
‘’Tunaumia sana
kutokana na tunachangishwa ela kila siku
lakini mabadiliko hakuna, huwa kuna
bomba likipasuka maji yanajaa na
kusababisha mashimo na magari yetu
yanazidi kuumia alafu pesa nyingi
tunatoa hamna mabadiliko yoyote katika
kituo hiki,’’ Alisema mmoja wa madereva hao.
Wakati huo mwandishi wetu ilijaribu kwa hali na
mali kuwatafuta wa husika na ilipofika
ofisi za kituo hicho wahusika
hawakuonesha ushilikiano huku ofisi hizo zikionekana kufugwa licha ya wahusika
kuwepo mahali hapo .
Kituo cha daladala cha tegeta nyuki kilianzishwa lasimi mwaka 2013.,Licha ya
kuwepo kwa changamoto kadhaa zinazokabiri kituo hicho bado kimendelea kuwa kitovu cha usafiri kwa wakazi wa tegeta
na maeneo ya kando kando kutokana na kupatikana kiurahisi usafiri wa kuwapeleka
sehemu tofauti tofauti za katikati ya mji na maeneo mengine ya jiji la Dar es
salaam.
No comments:
Post a Comment