Thursday, 27 October 2016

UTALII WA NDANI BADO NI KIKWAZO



Na Fatuma Sultani

Utalii wa ndani bado ni kikwazo kwa wananchi kutokana na kulipa hela kubwa ya kiingilio pindi watakapo kutembelea vivutio vilivyopo nchini kwao.Hilo limejitokeza hivi karibuni ambapo chuo cha uandishi wa TSJ kilipokwenda kutembelea hifadhi ya taifa NGORONGORO na kutozwa hela kubwa tofauti na matarajio yao.


Tukio hilo liliibua maswali kwa walimu na viongozi wa serikali ya wanafunzi wa chuo hicho na kusema hela wanayotakiwa kulipa ni nyingi na kwa mwananchi wa kawaida hataweza kumudu gharama hiyo ya shilingi elfu kumi na moja na mia nane kwa kila mmoja kwani hii huwanyonya wananchi na sio kuwapunguzia gharama.



Akiongea na chombo chetu cha habari bw.GEORGE BARTAZARY mwalimu wa chuo hicho alisema serikali inabidi kupunguza gharama za utalii wa ndani na kuwafanya wananchi kutembelea sehemu hizo ,kwani bila ya kufanya hivyoo utalii wa ndani utazidi kudorora na kutopata mapato mazuri juu ya utalii wa ndani na kuwafanya wale wenye hela ndio watakaofaidika na jambo hilo.


Na pia makamu wa rais wa chuo hicho Bi.FATUMA SULTAN alisema walipata shida sana kwenye swala zima la malipo kwani hela ilikuwa kubwa tofauti na bajeti waliyoipanga Na kufanya kupata wakati mgumu juu ya swala hilo.
.

Mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro iliisema kuwa  wao huwa hawategemei serikali huwa wanajimudu wenyewe bila kutegemea pato lolote lile kutoka serikalini na kutokuweza kupunguza gharama za viingilio pindi mwananchi anapotaka kutembelea hifadhi hiyo ya taifa NGORONGORO.



Serikali inabidi kuangalia hili swala kwa jicho la tatu kwani wananchi huzidi kuumia juu ya jambo hili .Na kuwapunguzia bei ili kufanya kila mmoja kujivunia na kuweza  kutembelea vivutio vilivyopo nchini mwao haswa TANZANIA .

No comments:

Post a Comment