Wednesday 26 October 2016

MFEREJI WA MALAPA WAKARABATIWA

Na Richard Y Kasaini

Baada ya matatizo ya mafuriko kwa muda mrefu Serikali imeamua kujenga mifereji imara ili kuweza kuepukana na mafuriko.Tukio hilo limechukua nafasi katika mfereji mkubwa ambao hukusanya maji yake katika mto Msimbazi ambao ndio mto mkubwa hapa Dar es salaam.

Serikali ya manspaa ya ilala imeamua kujenga mfereji maalumu ili kuepusha mmomonyoko wa udongo na mafiriko.Ujenzi huo ambao umeanzia eneo la Buguruni Malapa katika mfereji ambao unapeleka maji yake katika mto Msimbazi mto ambao hupokea kiwango kikubwa cha maji katika mji wa Dar es salaam.
GARI MAALUMU KWA AJILI YA KUCHIMBIA ARDHI LIKIWA LIMEEGESHWA

Katika ujenzi huo ambao mpka sasa gharama yake bado haijawekwa wazi.Ujenzi ambao inasemekana utamalizikamwezi ujao hayo yalisemwa na mkandarasi ambaye amepewa dhamana ya kusimamia shughuli hiyo mpaka mwisho ujenzi utakapokamilika na kukabidhi kwa mhe Paul Makonda.
MOJA KATI YA MADARAJA AMBAYO MFEREJI WA MALAPA INAPITA

Mkandarasi huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la bw Humfrey alikieleza chombo hichi kuwa ujenzi huo upo mbioni kukamilika kwani wanatakiwa kufanya haraka kwani kipindi cha masika kinakaribia na huenda mvua za mwaka huu zikawa kubwa ndio maana serikali imeamua kujenga mfereji huo ambao inasemekana ndio mfereji mkubwa zaidi hapa jijini.
Baadhi ya wanachi waishio karibu na mfereji huo wameeleza kero zao za muda mrefu na wengi wakionesha kuridhishwa kwa ujenzi wa mfereji huo kwani mmomonyoko wa udongo utapungua kwa kiasi kikubwa.
BAADHI YA NYUMBA AMBAZO ZILIPATWA NA MATATIZO YA MAFURIKO KABLA YA UJENZI KUANZA

Licha ya wananchi hao kufurahishwa na ujenzi huo wengine wameonesha kukasirishwa kutokana na uchelewashwaji kwani huko nyuma madhara yalikuwa ni makubwa sana hasusan katika maeneo yanayopakana na mfereji huo ambao umechukua eneo kubwa sana la ardhi.Na inaonesha wazi kuwa ikitokea mafuriko wakazi hao ndio ambao hukumbwa zaidi na matatizo hayo kwani wao ndo wapo jirani na mazingira hayo.
KIPANDE MOJAWAPO AMBACHO UKARABATI WAKE UNAENDELEA

No comments:

Post a Comment