Thursday 27 October 2016

KERO WA MACHINGA SOKO LA MIDIZINI

Na Tekla Zakaria
Hali ambayo inaleta tafarani kwa watembea kwa miguu katika barabara ya soko hilo kuwa msongamano wa watu na magari.

 Soko hilo ni njia kubwa kwya watembea kwa miguu lakini sasa imekua nisehemu ya wamachinga kupanga kupanga biashara zao katikati ya barabara na kusababisha kuwepo kwa foleni za magari na watu pia.

 Mwandishi wetu aliongea na mama mmoja ambaye alifahamika kwa jina la amina alisema hali hiyo inawafanya wapate hofu pindi watoto zao wanapotoka nje kucheza wakiamini wanaweza kupotea na hata kugongwa na gari

Aidha alisema mama huyo kuwa wamachinga waweza kufanya biashara zao katika meza husika au kupata sehemu maalum kuuzia kama masoko mengine.
Hivyo wameiomba serikali kuchukua jukumu lake la kuwatimua wale wanaofanya biashara zao chini kwa kupunguza msongamano na kuwataka wawe na meza rasmi kama wafanya biashara wengine wa soko hilo.

Pia hali hii itawaweka raiya wanao ishi maeneo ya karibu na soko hilo kuwa na amani pale waototo wao watokapo kucheza bira kupata dhoruba yoyote kwa watu na usafiri kwa eneo hilo.


No comments:

Post a Comment