Thursday, 27 October 2016

WANAFUNZI WA TSJ WAFURAHIA ZIARA YA KIMASOMO



Na ANITHA JAIL
 
Ziara iliyoandaliwa na serikali ya wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari TSJ kilichopo Dar es es salaam Ilala kimefanikiwa kutembelea sehemu walizopanga jijini Arusha.


Makamu wa Raisi wa chuo hicho Fatuma Sultani amesema anawashukuru sana wanafunzi  na walimu wote ambao walikuwa pamoja mwanzo mpaka mwisho wa safari bila matatizo yoyote.
 
Mbali na hayo wanafunzi walipata nafasi ya kufahamiana sababu muda mwingi walishinda pamoja wakitembelea sehemu mbalimbali za vivutio na redio(Sunrise FM
Ziara imetusaidia kimasomo kiujumla lakini tumeona vivutio kama wanyama,milima n.k pia kuna mambo mengi tulikuwa hatuyajui na baadhi ya wanafunzi walikuwa hawajawai kufika alisema mmoja wa wanafunzi
 
Wazazi au walezi waunge mkono kuhusu ziara za kimasomo zinazoandaliwa ili wanafunzi waweze kujifunza vitu vingi ambavyo hawavijui ili kuweza kuongeza ujuzi kwenye fani ya uandishi wa habari.

No comments:

Post a Comment