Friday 28 October 2016

WAFANYABIASHARA YA NYANYA SOKO LA ILALA WALIA NA KUSHUKA KWA BEI



Na Msafiri Mohamed

Wafanyanyabiashara ya nyanya katika soko la ilala lililopo jijini Dar es salaam walalamika na kupolomoka kwa bei  ya nyanya sokoni hapo katika msimu huu wa mavuno na kupelekea kushuka kwa hali ya biashara ya biashara ya nyanya sokoni hapo
 
mmoja  wa wafanyabiashara akiwa amepumzika
Hayo yalibainika baada ya mwandishi wa habari hii kutembelea soko la ilala na kujionea hali hiyo  na kujionea  mazao ya chakula yakiwa mengi na kuharibika


Mwandishi wetu  alitaka kujua hali ilivyo sokoni hapo hasa kwa  mazao mbogamboga yakiwemo nyanya ,vtunguu,viazi ndipo tulipo mpata  muuzaji wa mmoja wa nyanya  ambaye hakutaka kutajwa jina lake ndio  alipoongea na waandishi  akasema hali kwa sasa ni ngumu kutokana  na kiasi kikubwa cha nyanya kinachoingia sokoni hapo kila siku na kupelekea mlindikano wa bidhaa hiyo na kupelekea kushuka thamani.

picha ikionyesha watu wachache wakiwa sokoni kwa ajiri ya kufuata mahitaji

 Na kuongeza kuwa hali hiyo huwa inajitokeza katika kipindi cha msimu wa mavuno ya nyanya ambapo hupelekea kushuka kwa bei kutokana na upatikanaji wa bidhaa hiyo kuliko mahitaji yake halisi.  

No comments:

Post a Comment