NA SABORE LAIZER
Watanzania wakumbushwa kukuza Utalii wa
ndani ili waweze kuvitangaza vivutio vilivyomo nchini kwa Watalii kutoka nje,
alisema Bwana Johaness Japheth katika mamlaka ya ngorongoro
akiongea na Wanafunzi wa chuo cha Time school of Journalism cha jijini Dar es
salaam .
(muongozaji wa hifadhi ya ngorongoro bwn johanes akiongea na wanafunzi wa tsj) |
Bwana Japhet aliongeza kwamba wanapokea
wageni wengi kutoka nje ya nchi, mwamko ni ndogo sana kwa wazawa hii
inachangia watanzania kushindwa kutangaza vivutio vilivyomo nchini.
Naye afisa utalii wa mamlaka hiyo ndugu
Moinga lesasi alisema kuwa viingilio vinafikika kwa kila mtanzania kwa
watoto kuanzia miaka mitano mpaka kumi na saba ni shilingi 2600 na mtu
mzima ni 11800 hii ni baada ya mwaka wa
fedha kuanza yaani 2016/2017 .
(Wanafunzi wa TSJ wakielekea ndani ya kreta
ya Ngorongoro
Pia aliongeza kuwa kuna gari maalumu
kwa watanzania kuingia kreta ya ngorongoro kwa kuchangia mafuta lita mia moja
ili kurahisisha kufanya mzunguko (game drive).
Wanafunzi wa chuo cha Time school of
Journalism walionekana kufurahia ziara hiyo ya masomo baada ya kumaliza
Mizunguko ndani ya kreta ya ngorongoro waliendelea kuuliza maswali kwa
mwongozaji bwana Johaness wakitaka kujua utofauti za nyakati za masika na
kiangazi kwa watalii
(Baadhi ya vivutio
vinavyopatikana ndani ya Ngorongoro)
Hifadhi ya ngorongoro ni ya kipekee
duniani kutokana na vivutio vilivyomo, watalii wanaingia kila kila siku na
wengine hupenda kufanya sehemu ya kimasomo hivyo tunapokea taasisi nyingi za
elimu
No comments:
Post a Comment