Na Christian John
Baada ya mchakato wa muda mrefu wa kumtafuta
Meya wa Wilaya mpya ya Ubungo kufikia tamati katika hali ya kushangaza madiwani toka chama cha CHADEMA wamesusia
uchaguzi huo.
Aidha uchaguzi huo uligubikwa na wingu zito
mara baada ya waandishi wa habari kuzuiwa kuingia katika ukumbi wa uchaguzi
jambo lililoleta mkanganyiko kwa wananchi kwa kukosa habari muhimu ambazo ni
haki yao.
Akizungumza kwa hisia kali Mh.Diwani wa Mbezi
Beach Florence Lupomo amesema kuwa walikuwa ukumbini hapo kutoa sapoti kwa
madiwani wenzao ili kuhakikisha UKAWA inamiliki jiji lakini kwa kile
alichokiita hujuma za CCM kuwarudisha nyuma kwa kufanya maamuzi ya ajabu.
“Huu ni uhuni aisee Ndalichako amefuata nini
huku yeye yupo Ilala ameapa huko kama diwani huku hatumjui sisi,inauma sana
kuona tunaonewa ila hatukubali kabisa”
Kwa upande wa Chama cha mapinduzi wao
waliendelea na uchaguzi huo huku mtoto wa aliyekuwa spika wa Bunge Samuel
Sitta,Benjamin Sitta akiibuka kidedea wa uchaguzi huo.
Chama cha Chadema kimetoa tamko na kusema
kitapeleka suala hilo mahakamani.
No comments:
Post a Comment