Na Alfredy Geofrey Mhagama
Wafanyabiashara
wa soko la Buguruni ililopo katika Wilaya ya Ilala jijini Dar Es Salaam
wamelalamika baada ya bei ya nyanya kushuka na kupelekea kupata hasara huku
wanunuzi kwa upande wao ikiwa ni furaha.
Wafanyabiashara
hao wameeleza kuwa Mkoa wa Dar Es
Saalaam unategemea nyanya kutoka nje ya mkoa
hivyo inawalazimu wao kununua kwa bei ya juu na kuuza kwa bei ya hasara
ambapo tenga uuzwa kwa sh 52,000 hadi kufikia sh 40,000.
Akizungumza
na mwandishi wetu mfanyabiashara Juliana Kimaya alisema "Biashara ya
nyanya sasa imekuwa hasara kutokana wakulima kuunza kwa bei ya juu kwa
wafanyabiashara huku bei ya sokoni ni dogo na endapo utapandisha bei nyanya
zinakuozea"
Pia Shabani
Njore alisema kuwa bei ya nyanya imeshuka kwa sasa pia hata wateja ni wachache
sana na nyanya ni nyingi sokoni hali inayopelekea nyanya kuozea sokoni na
kupata hasara au kuuza tu kwa bei ya chini ili kuebusha hasara kubwa.
Kwa upande
wa wateja sokoni hapo wamesema kwa sasa bei ya nyanya ni ya kawaida ambayo kila
mtu anaweza kununua kuliko hapo mwanzoni ambapo bei ilikuwa juu sana .
Aidha kwa
wafanyabiashara wa nyanya sokoni hapo wameiomba serikali kuwajengea kiwanda cha
kusindika mazao ya mbogambaga ili kuondoa hasara wanayoipata kutokana kushuka
kwa bei ya nyanya na kukosa wateja pia kwa wingi na kupelekea nyanya kuoza
zikiwa sokoni.
No comments:
Post a Comment