Na Alfredy Geofrey
Mhagama
Imeelezwa
kuwa moja ya sababu ya kuanzishwa kwa shule ya msingi Laiboni iliyopo
katika kata ya Makuyuni Wilaya ya
Monduli Mkoani Arusha ni kufatia kifo cha moja ya mtoto wa mganga wa jadi wa jamii ya kimasai aliyefahamika kwa jina la
Meshuke Mapi kukongwa na gari alipokuwa akielekea shule ya msingi Eslaley.
Hayo yalielezwa
na mwalimu Mkuu wa shule hiyo ya msingi Laiboni Bi Rogatha Mbuyaalipokuwa
akizungumza na wanafunzi wa chuo cha Times school of jounalism kilichopo jijini
Dar Es Salaam.
Bi mbuya aliongeza kuwa baada ya kifo cha mtoto wa
mganga huyo wa jadi aliamua kuanzisha shule yake binafsi ili watoto wake na
wajuu zake wote waweze kusoma hapo ambayo ilianza mwaka 1997 wanafunzi wakiwa
wanasomea chini ya mbuyu.
Pia bi Mkuya
alisema kuwa shule hiyo ilipokuwa ikianzishwa watoto wa Mzee Meshuke ndio
walikuwa walimu, alifanikiwa kujenga darasa moja pamoja na ofisi na baadaye
shule hiyo ikasajiliwa na kuchukiliwa na serikali mwaka 2007 ambapo katika
shule hiyo zaidi ya asilimia 90 ya wanafunzi ni watoto, wajukuu na vitukuu vya
mzee huyo.
Sanjari na hilo
pia Mkuu huyo wa shule ya msingi Laiboni Bi Rogatha Mkuya aliweza kupokea
msaada kutoka kwa wanafunzi pamoja na walimu wa chuo cha Times School of
journalism [TSJ] ikiwemo Madaftari,kalamu,sabuni ya mche pamoja na sabuni ya
unga box moja
.
vilevile
wanafunzi hao na walimu waliweza kuchangia kiasi cha pesa pia kutoka kwa kila
wanafunzi kufatia bi Mkuya kueleza changamoto mbalimbali zinazokabili shule
hiyo ikiwemo ukosefu wa maji wakati wa kiangazi hali inayopelekea wanafunzi
kukosa chakula shuleni,pia upungufu wa madarasa mawili ya kufundishia.
No comments:
Post a Comment