Na Fadhili Kijanjali
Club ya mpira ya Iringa inayokipiga
ligi daraja la kwanza maarufu kama Lipuli jana imeambulia kichapo cha bao3 kwa0
kutoka kwa Friends Ranges yenye makazi yake jijini Dar es salaam katika mechi za mizunguko zinazoendelea.
Kikosi cha Lipuli kabla ya mchezo kuanza hapo juzi uwanja wa karume jijini Dar es salaam |
Club ya Lipuli ilianza kwa kasi
mchezo huo huku ikionekana kuwazidi uwezo Friends Ranges na kumiliki mpira kwa
kiasi kikubwa sana katika dakika za mwanzo nakuonyesha wazi kuwa wanaweza
kuushinda mchezo huo.
Vijana wa Friends Ranges wakisali kwa pamoja kabla ya mechi yao dhidi ya Lipuli uwanja wa karume jijini Dar es Salaam |
Baada ya dk15 za mchezo huo club ya
Friends Ranges ilijiandikia bao la kwanza kupitia kwa mchezaji wao Almasi
Mkinda aliyevalia mgongoni jezi namba 19 bao lililowafanya lipuli kuzidiwa kwa
kiasi kikubwa baada ya bao hilo.
Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika
lipuli walikuwa nyuma kwa bao1 huku Friends Ranges wakiongoza
Kipindi cha pili kilianza kwa pande
zote mbili kutoshana nguvu na dk ya 68 Friends Ranges wakajiandikia bao lao la
pili kupitia kwa Fred Cosmas aliyevalia jezi no3 mgongoni nakuwafanya Lipuli
kupoteza mwelekeo wa mchezo huo.
Kocha wa Friends Ranges Edward Christopher akizungumza na wachezaji wake wakati wa mchezo dhidi ya lipuli uwanja wa karume jijini Dar es salaam |
Khali hiyo iliwafanya Lipuli kupotea
kabisa kabisa mpaka dk90 za mchezo huo, na ndani ya dk4 za nyongeza Rangers
wakajiandikia bao lao la tatu kupitia kwa mchezaji wao Isihaka nakufanya mchezo
huo umalizike kwa Lipuli kuambulia kichapo cha bao3.
Wachezaji wa Friends wakishangilia bao lao walilolipata katika dakika za nyongeza kupitia kwa mchezaji wako Isihaka uwanja wa karume jijini Dar es salaam |
Kwa upande wake kocha wa Friends
Ranges Salvatory Edward amesema lipuli kucheza mpira mwingi haikuwa kigezo cha
yeye kukosa ushindi kwakuwa aliamin vijana wake wana mbinu nyingi za ufungaji.
No comments:
Post a Comment