Na Peter Mhina
Hali ya
usafi ya soko la buguruni yaimarika baada ya halmashauri ya manispaa ya ilala kusimamia kikamilifu zoezi la usafi katika soko hilo. Baada ya kuweka watu maarumu ambao wanahakikiasha hakuna taka zinazo zagaa ovyo katika
mazingira wanayo fanyia biashara.
Mwanzoni soko hilo lilionekana
kama halina usimamizi mzuri baada
ya kuwepo taka kila eneo na maji machafu yanayotuwama hususani wakati wa
mvua nyingi,na kusababisha harufu mbaya katika eneo hilo la soko.
MOHAMED
ULONGO ni mfanya biashara alisema " tunaishukuru serikali kwa kijumla kwa kuzingatia usalama wa
raia na mali zao hasa katika soko letu hili la buguruni na sasa kumekuwa na
hali nzuri katika maeneo yetu ya kazi
kumesaidia kuepukana na magonjwa ya milipuko hasa kuptia biashara tunayo
ifanya katika shughuli zetu za kilasiku katika kuzalisha kipato".
Hivyo nachukua nafasi hii pia kuwa
hamasisha wafanya biashara wenzangu
kufanya usafi katika maeneo yetu ya kazi
hasa katika maeneo yetu kuepukana na magonjwa ya milipuko
Hata
hivyo wafanyakazi hao wameishauri serikali katika kuhamasisha wananchi
wanaofanya kazi katika mazingira yenye mkusanyiko wa kazi katika masoko .,na vituo
vya daladala kuweza kutunza mazingira,
No comments:
Post a Comment