Aliyekuwa
kocha wa Yanga Hans Plujim ambaye alishindwana na timu hiyo na kuamua kuachana
na timu hiyo ambayo ilionekana kama kutoaanza vizuri msimu huu chini ya Hans
Baada ya
makubalaino ya Hans na Yanga ndio kocha huyo alisema kuwa Yanga wanakazi kubwa
sana ya kufanya msimu huu kwani wapinzani wao Simba siyo wa mchezo mchezo.
Hans ambaye
alizungumza na gazeti hili wiki moja iliyopita alisema kuwa anawatakia kila la
heri timu yake ya zamani Yanga lakini wanakazi kubwa ya kufanya ili kuwazidi
wapinzani wao Simba
‘’ Simba
msimu huu wamejipanga sana na nataka kuwaambia kitu tena kwa kuwakumbusha
wapenzi, mashabiki, wachezaji na viongozi kwa ujumla wanakazi kubwa ya kufanya
ili kuweza kulitetea taji lao ambalo walilinyakua msimu uliopita’’alisema Hans
‘’Siyo kama
nawatisha ila nimeiona Simba kuwa wapo vizuri na wanania ya dhati kuona
wanakuwa mabingwa msimu huu kwani hawataki mchezo mchezo kabisa katika kila
mechi zao kama msimu uliopita huku wakiwa na kikosi bora tofauti na msimu
uliopita’’alisema
Hata hivi
Simba watakuwa na kibarua kingine siku ya kesho katika uwanja wa Kambarage kuwakabili Mwadui fc, ambao wanaangaika
kupata matokeo msimu huu.
No comments:
Post a Comment