Na Fadhili
Kijanjali
DAR ES
SALAAM
Katika
mchezo wa kuendelea na mzunguko wa ligi daraja la kwanza kwa mechi za kundi A
hapo jana katika uwanja wa karume jijini dar es salaam timu ya Police Dar na
Ashanti United jana zimetoshana nguvu kwa kutoka suruhu ya bao2 kwa2.
Kikosi cha Police Dar kabla ya mchezo kuanza katika uwanja wa karume jijini Dar es salaam |
Police
walikuwa wa kwanza kuandika gori katika mchezo huo dakika ya 40 kupita kwa
mshambuliaji wao Hamadi Kambagwa bao lililowafanya police kumaliza kipindi cha
kwanza wakiwa mbele kwa bao moja kwa bila.
Kipindi cha
pili cha mchezo kilianza kwa kasi na Ashanti uonesha uwezo mkubwa nakuongeza
mashambulizi hali iliyowafanya Ashanti kujipatia penalty dakika ya 75 iliyojazwa
nyavuni na mshambuliji wa timu hiyo Yahaya Zaydi aliyevalia jezi nambari13.
Mshambuliji wa Ashanti United Yahaya Zaydi akitupia nyavumi mpira wa penalti uwanja wa karume jijini Dar es salaam |
Dakika tano
baadae Ashanti waliandika bao lakuongoza mchezo huo kupitia kwa mshambuliaji
wao machachali Yahaya Zaydi aliyetupia bao hilo kwa kichwa Zaydi alionesha
uwezo mkubwa katika mchezo nakuwasumbua walinzi wa Police Dar.
Wachezaji wa Ashanti United wakiomba dua kwa pamoja kabla ya mchezo kuanza kwenye uwanja wa karume jijini Dar es salaam |
Dakika ya 86
ya mchezo huo mambo yalibadilika nakuwafanya walinzi wa Ashanti kukubali suruhu
baada ya mshambuliaji wa Police Evance Alfred kuandika bao lakusawazisha
lilifanya mchezo kumalizi kwa sare ya bao 2 kwa 2.
Kwa upande
wa makocha wa timu zote mbili wamelalamikia uwezo mdogo wa waamuzi unaoneshwa
na waamuzi wanachezesha michezo ya ligi daraja la kwanza nakuongeza kuwa
waamuzi hao huchangia michezo kuwa migumu.
Waamuzi wa mchezo kati ya Police Dar na Ashanti United wakizungumza kabla ya mchezo huo kuanza uwanja wa karume jijini Dar es salaam |
No comments:
Post a Comment