Na fadhila
mohamed
Kutokana na mazingira ya soko la buguruni
lilulopo katika manispaa ya wilaya ya ilala jijini dar es salaam kutokuwa katika hali ya usafi ni kero kwa
wananchi wa karibu kutokana na
mrundikano wa maji machafu yanayokusanyika wakati wa mvua
sehemu ya mbela sokoni hapo ambapo magari hupakiwa |
.
Mmoja wa wakazi wa eneo hilo la karibu
anaejulikana kama juma mzaramo alieleza kuwa miundombinu ya kupitisha maji
taka sokoni hapo ni mibovu kwa kiasi
kikubwa kwani husababisha maji kutapakaa kila eneo na hatimaye huoza na kuanza
kunuka .
Licha ya wakazi hao kulalamika lakini pia
baadhi ya wateja na wafanyabiashara sokoni
hapo wanakerwa na kitendo hicho ambacho kinasababisha hali ya hewa kuwa
mbaya baadhi ya maeneo kuzunguka soko hilo.
Hii ni moja sehemu ya nyuma sokoni hapo ambayo maji hutuama wakati wa mvua |
Kwa upande wake mwenyekiti wa soko hilo yeye
alithibitisha kuwepo kwa kero nyingi sokoni hapo na kuwaomba wakazi wa karibu
kuthibiti babadhi ya watu wanaokuja kutupa taka sokoni na kushirikiana katika
kulinda usafi .
Aliendelea kusema kuwa matatizo haya
yanajulikana na manispaa na yapo katika ripoti ya utekelezaji wa kero hizo.
No comments:
Post a Comment