Ziara ya Masomo yatoa
ajira.
Na Paulo Thomas.
Kufuatia ziara ya
kimasomo ya chuo cha uandishi wa habari Time school of Journalism
katika Kampuni ya IPP Media
upande wa uchapishaji wa gazeti la the Guardian iliyopo Mikocheni Dar es salaam
imeibua fursa ya ajira katika Tasnia hiyo.
Akitoa utangulizi Ofisa mahusiano
wa Kampuni hiyo ya IPP Media Anthony Mgeni alipokuwa anazungumza na
wanafunzi hao wiki iliyopita alisema
“vijana wanatakiwa
kutambua fursa za ajira hili kuweza kuondokana na changamoto za ajira hapa
nchini”.
Hata hivyo alisema kuwa
kujitambua pamoja na kujiamini kunaweza
kumfikisha mtu katika malengo na ndoto alizojiwekea kwa kuhakikisha kuwa ana
amini juu ya kile anachokifanya.
Pia alitoa ufafanuzi
juu ya namna wanavyotoa fursa mbalimbali
kwa wana tasnia ya uandishi wa
Habri na utangazaji ili kuweza kupata uzoefu wa tasnia hiyo na baadae kuweza
kushinda na soko la ajira.
Baadhi ya wanafunzi
katika ziara hiyo walitoa shukrani kwa uongozi wa Kampuni hiyo kwa fursa ambazo
hutoa kwa wanafunzi kwa ajili ya kuwa na mazoezi ya vitendo ambayo huwajengea
uzoefu wa kazi zao.
Hata hivyo mratibu wa
masomo wa chuo cha Time School of Journalism Madam Blandina Semaganga
alieyeongozana na wanafunzi hao alitoa shukrani za dhati kwa uongozi wa IPP
Media kwa kuwapa nafasi yakufanya ziara
hapo.
Mbali na shukrani hizo
Madam Semaganga aliahidi kutoa ushirikaino wa hali na mali na uongozi wa kampuni hiyo ili kuweza kutumia
fursa za wanafunzi kwenda kufanya mazoezi ya vitendo katika Media hiyo kwa
ajili ya kupata fursa mbalimbali za ajira.
Mhariri wa Gazeti la
The Guardian Charles Mkude akizungumza na wanafunzi (hawapo pichani)katika
ziara hiyo.
Msanii maarufu na
mchora katuni Abdul Kingo akibadilishana mawazo na wanafunzi wa TSJ.
No comments:
Post a Comment