Wednesday 26 October 2016

WANACHI WALALAMIKIA UWEPO WA MAGARI KATIKA ENEO LA MAKABURINI

Na Richard Y Kasaini

Wananchi wa maeneo ya Buguruni manispaa ya Ilala wamelalamikia uwepo waeneo ambalo sio rasmi la maegesho ya magari ambalo lipo karibu na makaburi ya kikristu yaliyopo maeneo hayo kwani ni kama kutokuheshimu watu waliopumzishwa mahala hapo.
BASI LIKIWA LIMEEEGESHWA NA PEMBENI KUKIWA NA MATAIRI AMABAYO HUENDA NI TAKATAKA NA NYUMA YA ENEO HILO YAKIWAMO MAKABURI
.
Shughuli za uegeshaji wa magari maeneo karibu na makaburi yaliyopo Buguruni imekuwa kero kwa baadhi ya wananchi waishio maeneo ya karibu na maeneo hayo.Wananchi hao wametoa kero zao katika chombo hichi madereva wanaoegesha magari hayo katika mazingira hayo huenda wakawa hawajui dhamani ya watu waliopumizika katika eneo hilo.
MAGARI YAKIWA YAMEEGESHWA ENEO AMBALO MAKABURI YAPO HUKU MENGINE YAKIOSHWA HAPO
Licha ya malalamiko hayo kutoka kwa wananchi hao.Mmoja kati ya madereva hao anayeendesha gari aina ya coaster yenye namba za usajili T 487 BRZ inayofanya safari zake kutoka Buguruni kwenda Muhimbili aliyejitambulisha kwa jina la ALLY MAJALIWA alisema kuwa manispaa ya jiji la Dar es salaam ilipaswa kujenga uzio ambao ungeweza kuweka makaburi hayo katika hali ya usalama zaidi na kuepukana na malalamiko kutoka kwa wananchi wanaoishi mazingira hayo na walioipumzisha miili ya ndugu zao katika maeneo hayo.

Ukiachilia uegeshaji wa magari katika maeneo hayo lakini kumekuwa na shughuli mbalimbali zinazoendelea katika mazingira hayo kama kufyatua matofari,uoshaji wa magari na gereji.Huenda shughuli hizi ndizo zinazopelekea kuwepo kwa magari mengi katika maeneo hayo.

MAKABURI KATIKA MUONEKANO WA NYUMA AMBAKO MAGARI YAKIWA YAMEPAKI MBELE YAKE

Chombo hichi kilibahatika kukutana na moja kati ya viongozi wa maeneo ya ILALA SHARIFUSHAMBA aliyejitambulisha kwa majina DEVOTHA KAMUGISHA alisema kuwa serikali yake inatambua uwepo wa magari katika maeneo ya makaburi hivyo wapo katika harakati za kujenga uzio ikiwezekana kuhamisha baadhi ya shughuli zisizo na ulazima wa kuwepo katika maeneo hayo ambayo kiimani yanastahili heshima yake.

Mimi na wewe huenda tusijue kwanini jitihada za kuweka hata uzio zichelewe na kwanini maeneo kama haya yanapuuzwa sana.Majibu ya maswali haya yatajibiwa pale ambapo tutakapoona vitendo vikichukua nafasi na sio maneno ya ahadi za kila siku.
BAADHI YA SHUGHULI ZINGINE ZINAZOENDELEA MAKABURINI HAPO NI PAMOJA NA UFYATUAJI WA MATOFALI KAMA INAVYOONEKANA PICHANI

No comments:

Post a Comment