Na Alfredy Geofrey
Mhagama
Imeelezwa
kuwa moja ya sababu ya kuanzishwa kwa shule ya msingi Laiboni iliyopo
katika kata ya Makuyuni Wilaya ya
Monduli Mkoani Arusha ni kufatia kifo cha moja ya mtoto wa mganga wa jadi wa jamii ya kimasai aliyefahamika kwa jina la
Meshuke Mapi kukongwa na gari alipokuwa akielekea shule ya msingi Eslaley.
Pia bi Mkuya
alisema kuwa shule hiyo ilipokuwa ikianzishwa watoto wa Mzee Meshuke ndio
walikuwa walimu, alifanikiwa kujenga darasa moja pamoja na ofisi na baadaye
shule hiyo ikasajiliwa na kuchukiliwa na serikali mwaka 2007 ambapo katika
shule hiyo zaidi ya asilimia 90 ya wanafunzi ni watoto, wajukuu na vitukuu vya
mzee huyo.
Sanjari na hilo
pia Mkuu huyo wa shule ya msingi Laiboni Bi Rogatha Mkuya aliweza kupokea
msaada kutoka kwa wanafunzi pamoja na walimu wa chuo cha Times School of
journalism [TSJ] ikiwemo Madaftari,kalamu,sabuni ya mche pamoja na sabuni ya
unga box moja.
[Wanafunzi wa Times School of Journalism wakiwa wanaelekea katika Shule ya msingi Laiboni kutoa msaada] |
vilevile
wanafunzi hao na walimu waliweza kuchangia kiasi cha pesa pia kutoka kwa kila
wanafunzi kufatia bi Mkuya kueleza changamoto mbalimbali zinazokabili shule
hiyo ikiwemo ukosefu wa maji wakati wa kiangazi hali inayopelekea wanafunzi
kukosa chakula shuleni,pia upungufu wa madarasa mawili ya kufundishia.
[Rais wa Chuo cha Times school of journalism Sabore Laizer akimpatia mwanafunzi madaftari shuleni hapo] |
No comments:
Post a Comment