Na ANITHAN
JAIL
Shule ya
msingi Laiboni iliyoko mkoani Manyara wilaya ya Monduli imeanzishwa mwaka 1997
ikiwa na wanafunzi 9,mwanzilishi wa shule hiyo ni mganga wa kimasai.
Wanafunzi
hao ni wajukuu na watoto wake ambao wanaishi kwenye familia au maboma tofauti.Darasa
la saba mwaka wa kwanza walifaulu wanafunzi 12 na mwaka wa pili 19 bado mwaka
huu alisema mkuu wa shule hiyo mwalimu Regeto Mbuya.
Kutokana na
mganga huyo wa kimasai kupoteza binti yake aliamua kuanzisha shule iitwayo
Islelai na sasa inaitwa Laiboni na serikali kuamua kumuunga mkono
Mwalimu
Regeto alisema shule ina changamoto ya maji kwani wanategemea maji ya mvua na
mabwawa,na chakula kwani ardhi ya apo
hairuhusu kupanda mazao yoyote
Pia wazazi
wanachangia pesa ili watoto wao wapate chakula ambacho kinapikwa shuleni,na
walimu wa shule hiyo hawajaanzisha miradi ya kuwezesha wanafunzi kupata chakula
kwa haraka kwasababu ardhi ina mawe sana na wanyama pori kama tembo,fisi nk
Mratibu wa
masomo Madamu Semaganga pamoja na wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari TSJ walifika
shule apo wakiwa katika ziara ya kimasomo walichangai baadhi ya vitu kama
sabuni,miswaki,madaftari.
Serikali na
jamii kiujumla inabidi kuendelea kuunga mkono shule hiyo na kutoa misaada
mbalibali kwani bado ina changamoto nyingi
No comments:
Post a Comment