Thursday, 27 October 2016

BEI YAWALIZA WAFANYA BIASHARA SOKONI



Na Paul Thomas
Wakati Serikali ikiendelea kurekebisha Miundo mbinu na kuboresha huduma za jamii nchini, hali ni tofauti katika Soko kuu la vyakula la Ilala lililopo Wilaya ya Ilala Mkoa wa Dar es Salaam.

Hali hiyo imekuja baada ya wafanya biashara wa Soko hilo kulalamikia bei kupanda ghafla walipo kuwa wakizungumza na Mwandishi wetu hivi leo katika soko hilo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wafanyabiashara hao walisema hali ya biashara kwa sasa sio nzuri kutokana na bei wanayonunulia biadhaa kupanda tofauti na hapo mwanzo.

Mfanyabiashara mmoja wa nyanya aliyejitambulisha kwa jina la Masunga Elias alisema
“Kabati moja la nyanya walikuwa wananunua kwa shilingi elfu 10,000/= lakini kwa sasa bei imepanda na kufikia hadi elfu 15,000/= na kuwapa usumbufu kwa wateja wao waliozoea bei ya awali “ alisema.

Mwandishi wetu alipiga hodi hadi ofisi ya uongozi wa soko ili uweze kuzungumzia changamoto wanazokutana nazo ikiwemo bei kupanda lakini hadi anaondoka eneo la soko hakuweza kuonana na kiongozi yeyote na wala simu zao zilikuwa hazipatikani.





No comments:

Post a Comment