MRUNDIKO
WA TAKA WAZUA ZOGO TEMEKE.
Na
Paulo Thomas
Wananchi wa wilaya ya temeke wameilalamikia serikali
ya Mtaa kwa kuchelewa kupitisha gari la kubeba taka ambalo hupita kila baada ya
wiki, akizungumza na gazeti la TSJ mkazi wa eneo hilo aliyefahamika kwa jina la
Hassani Mohamed “alisema mtaa wao unaongoza kwa mazingira kuwa machafu kutokana
na Serikali yao ya Mtaa kutofuatilia magari ya Taka na kutokuchukua taka kwa
muda ambao umepangwa”.
Alisema swala hilo limekuwa ni kero kwa wakazi wa eneo hilo kutokana na taka kukaa muda mrefu
mitaani na kupelekea kutoa halufu kali na kushindwa kukaa kwa furaha, hata
hivyo mwenyekiti wa Mtaa wa Temeke mwisho Ndugu Jafari Iddi “alisema
wanashindwa kulifuatilia tatizo la usafi wa mazingira kutokana na Manispaa ya
Temeke kudai kuwa hilo swala watalisimamia kwa muda halafu watawaachia viongozi
wa Mtaa na matokeo yake mpaka leo
Serikali ya Manispaa haitaki kuachia
madaraka kwa viongozi wa Serikali ya Mtaa”.
Pia mwenyekiti huyo aliongeza kuwa swala la
magari kutokuchukua takataka kwa wakati ni
tatizo la sehemu ya kutupa takataka kuwa mbali, pia barabara
kuwa na mashimo hivyo magari kushindwa kupita kwa urahisi.
No comments:
Post a Comment