Na:-
Rahma Saidi
Wafanya
biashara wa soko la Pugu Kigogo freshi wamelalamikia uongozi wa soko kuhusu
suala la miundombinu kuwa mibovu na kusababisha biashara zao kuyumba kwa kiasi
furani.
Wafanya
biashara hao walisema kuwa kunatatizo la kutokuwepo na sehemu maalumu ya
kujisaidi haja kubwa na ndogo (choo) na kusababisha baadhi ya wafanya biashara
wengine kuacha kufanya biashara katika soko hilo.
Vilevile
walisema kuna baadhi ya viongozi wanalipelekesha soko kidikteta zaidi kwa
manufaa yao binafsi bila kujali haki za wafanya biashara hao.
Mmoja
wa wafanya biashara Bwana Sudi Hassani alisema kuwa wamejalibu kushtaki katika
uongozi wa soko hadi kwa diwani wa eneo hilo lakini bado hawakulifanyia kazi na
kuona halina umuhimu kwao.
Bwana
Sudi aliendelea kusema wanaumia na kuathilika hasa katika suala lakutokuwepo na
sehemu ya kujisaidia yaani vyoo.
Hata
hivyo mmoja wa viongozi Bwana Sospeter Mapanga alisema kuwa watalifanyia kazi
suala hilo kwa haraka zaid.
No comments:
Post a Comment