Na Imani
luoga
Madereva wa
mabasi jijini Dar es salaam wameiomba serikali kuboresha barabara ya kuelekea
kituoni hapo ambayo huchangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa magari.
Hii ni sehemu ya ndani ya kituo hicho cha mawasiliano ubungo |
Akizumgumza
na mwandishi mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya kinondoni MUSSA NATTY
amebainisha kuwa serikali inatambua tatizo la barabara hiyo na kuwa kwa
kushirikiana na benki ya dunia wameandaa mradi ambao utahusika kuboresha miundo
mbinu ya jiji la Dar es salaam.
Kwa upande
wao baadhi ya madereva wanaotumia kituo hicho wamesema kuwa ubovu wa barabara
hiyo umekuwa na tatizo kwa kipindi kirefu sana na tangu serikali iseme inatafutia ufumbuzi mpaka sasa
hakuna kinachoendelea alisema Hussein juma mmoja wa madereva.
Naye mmoja
wa watumiaje wa barabara hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Bwn.Ally Mohamed
mkazi wa sinza alisema “tunapata tabu
pindi tutumiapo barabara hii hasa wakati wa mvua kwani inajaa maji na kuwa na
mashimo marefu’’alisema mkazi huyo
Kituo cha
mawasiliano kilifunguliwa mwezi October 2014 mara baada ya kuhamishwa kutoka
katika eneo lililopo pembezoni mwa shirika la umeme Tanzania (TANNESCO).
No comments:
Post a Comment