Thursday 27 October 2016

LAIZER AWAMWAGIA SIFA WANAFUNZI WENZAKE



Na Fadhila Mohamed

       Rais wa chuo cha uandish wa habari kilichopo ilala sharif shamba ,time school of journalism(tsj)sabore lazier  amewapongeza wanafunzi wenzake wa ngazi ya stashahada ya nne  kwa kushiriki kiakamilifu katika safari ya kimasomo ijulikanayo kama study tour iliyofanyika mkoani  Arusha. 

      Kutokana na kuwepo kwa ziara hiyo ya kimasomo wanafunzi hao waliweza kujifunza mambo latika tasnia yao ya habari kama kuandaa vipindi ambavyo vitaelimisha jamii kuhusu utalii wa ndani ya nchi yao na pia utangazaji wa vipindi mbalmbali kama ilivyo ada ya wanfunzi chuoni hapo

        Safari hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kutembelea mbuga za wanyama ,vituo vya redio ili kujua  jinsi ya watangazaji wavyoendesha vipindi vyao  kama waandishi wa habari kwa kuwa wanahitimu mafunzo yao mwezi ujao.

      Kiongozi  huyo aliendelea kuwamwagia sifa wanafunzi  hao kuwa wameonesha  nidham kwake kama kiongozi  wa wanafunzi chuoni  hapo , na kuwasihi kuwa na moyo huo hadi watakapoondoka chuoni hapo mwezi ujao.

No comments:

Post a Comment