NA
:- Rahma Saidi
Wafanyabiashara
wadogowadogo wa soko la Buguruni jijini Dar es salaam walalmika kulipa ushuru
mkubwa.
Akizungumza na gazeti
la chipukizi leo mmoja wa wafanya biashara hao Bwana Ally Juma amesema kuwa
ushuru wanaolipa ni mkubwa kuliko biashara wanazofany, ‘ushuru tunaolipa ni sh.
500 ukiangalia mzigo ulionunua wiki nzima haujaisha hivyo unapouza kila unalipa
hadi mzigo uje kuishe faida inakuwa ndogo,’ alisema.
Aliendelea kusema kuwa
anaiomba Almashauri ya soko hili liwasaidie katika suala hilo kwani pesa
wanazopata ndizo zinawasaidia kukidhi mahitaji yao ya kila siku hivyo ipunguze
ushuru huo walipe elfu moja kwa wiki kwani ukipiga hesabu miatano kila siku kwa
wiki ni elfu tatu miatano.
Naye mtoza ushuru wa
soko hilo aliyekataa kutaja jina lake alisema kuwa wafanyabiashara hao
wanaonewa lakini sio kweli kwasababu ushuru huo ndio unasaidia mazingira ya
soko hilo yawe na salama.
Pia alisema kuwa ushuru wanaolipa wafanya biashara hao ni
mdogo, ‘kwasababu kuna wafanya usafi, magari ya taka, wazoa uchafu, na walinzi
watalipwa na nani hivyo ushuru wanaotoa ndio tunawalipa watu hao’ alisema mtoza
ushuru huo.
Haidha Halmashauri ya
soko hilo ilisema kuwa wafanyabiashara wadogowadogo wote wamaeruhusiwa kufanya
biashara zao na Mh. Rais hivyo hawatakiwi kusumbuliwa na walipe ushuru
kulingana na mapato yao.
No comments:
Post a Comment